• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • UTALII IRINGA
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

KILIMO KINACHANGIA ASILIMIA 85 YA PATO LA MKOA IRINGA.

Posted on: January 2nd, 2018


Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Sekta ya kilimo inachangia katika usalama wa chakula na utoaji ajira na uchumi wa Mkoa wa Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi ya Mkoa wa Iringa kwa wajumbe kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa waliofanya ziara ya mafunzo ya siku tano mkoani Iringa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa jana.

Masenza alisema “sekta ya kilimo katika Mkoa ni muhimili mkuu wa uchumi na inachangia katika usalama wa chakula na utoaji wa ajira. Sekta hii inachangia takribani asilimia 85 ya pato la Mkoa kwa mujibu wa wasifu wa kiuchumi na Kijamii, mwaka 2013”. Alisema kuwa lengo la Mkoa ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na chakula cha kutosha, wanaongeza kipato na uhakika wa upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda.

Akiongelea sekta ya mifugo na uvuvi, mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa Mkoa wa Iringa una mashamba makubwa ya mifugo 20 yanayomilikiwa na serikali na watu binafsi. Alisema kuwa mashamba hayo huzalisha maziwa, mitamba na madume bora.

”Mkoa wa Iringa hadi kufikia Juni, 2017 ulikuwa na jumla ya ng’ombe 330,372, mbuzi 160,227, kondoo 62,475, nguruwe 109,131 na kuku wapatao 1,341,718 na eneo linalotumika kwa malisho ni jumla ya hekta 209,003” alisema mkuu wa Mkoa.

Kwa upande wa uvuvi, alisema kuwa Mkoa una mabwawa madogo 1,893 yaliyochimbwa yanayotumiwa kwa shughuli za uvuvi. Alisema kuwa Mkoa una wavuvi 5,807 ambao hufanya shughuli za uvuvi kama mtu mmoja mmoja na katika vikundi. Mavuno ya samaki yamekuwa yakiongezeka kutoka Tani 913.50 mwaka 2011/2012 hadi kufikia Tani 1,186.99 mwaka 2014/15.

Kwa matokeo ya Sensa ya mwaka 2012 Mkoa wa Iringa ulikuwa na watu 941,238 kati ya hao wanaume walikuwa 452,052 na wanawake 489,186 na wastani wa ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka ni asilimia 1.1. Makadirio ya idadi ya watu kwa mwaka 2017 ni watu 1,000,040; wanaume wakiwa 480,293 na wanawake 519,747.

=30=



Matangazo

  • Ratiba ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa Mwezi Februari February 07, 2019
  • TAARIFA YA TATHMINI YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018 January 28, 2019
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019 Mkoa wa Iringa. December 17, 2018
  • Ratiba Ya Mh. Mkuu Wa Mkoa Kwa Mwezi January January 18, 2019
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MKOA WA IRINGA KUPATIWA MRADI MUHIMU WA KUKUZA UTALII

    February 04, 2019
  • RC ALLY HAPI AKUTANA NA WADAU WA UTALII MKOANI IRINGA

    January 24, 2019
  • RC ALLY HAPI AWASHUKIA MAKAMPUNI YANAYOKWEPA KULIPA KODI

    January 10, 2019
  • ORODHA YA WAPORAJI MALI ZA USHIRIKA IANDALIWE IRINGA

    October 16, 2018
  • Tazama zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA IRINGA BI.HAPPINESS SENEDA AKITEMBELEA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Press release
  • Completed projects

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2018, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.