Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi leo ameanza ziara ya kazi ya siku 5 mkoani Iringa kukagua miradi ya maendeleo. Ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake, RC Hapi leo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
Akiwa wilayani Mufindi amekagua miradi kadhaa ikiwemo mradi wa bwalo la chakula katika shule ya sekondari Mbalamaziwa wenye thamani *111,171,000,* Mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya iliyopo kijiji cha Igowole yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.
Miradi mingine iliyotembelewa leo ni pamoja na Zahanati ya kijiji cha Mtili na mradi wa hifadhi ya mazingira shamba la miti.
Pawaga Road
Postal Address: P.O.Box 858, Iringa
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2018 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.