Kikao kilifanyika katika Ukumbi wa Siasa na Kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 05/09/2019,lengo likiwa ni kujadili changamoto na kutoa maoni nini kifanyike ili kuboresha uwekezaji Mkoani Iringa.
Kikao hiki kimeongozwa na Mhe. Ally Hapi Mkuu wa Mkoa wa Iringa kama Mwenyekiti na Katibu Tawala wa Mkoa Iringa kama Katibu, pia Mhe. Richard Kasesela Mkuu wa Wilaya ya Iringa kama mwenyeji wa Wilaya. Pia kulikuwa na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Iringa na Wakurugenzi wote wa Wilaya za Mkoa wa Iringa, wadau wa maendeleo na wafanyabiashara wa Mkoni Iringa na wawakilishi mbalimbali kutoka Wilaya zote.
Taasisi kama TANTRADE, Benki Kuu ya Tanzania, RIFO, TPSF, TCIA pia zilikuwepo ili kujadili changamoto kwa pamoja na kutolea maoni nini kifanyike.
Akitoa utangulizi katika kikao hicho, Mhe. Hapi amesema, Baraza la Biashara la Mkoa wa Iringa ni ustawi wa maendeleo yetu ya Mkoa. Kutokana na kikao hicho kutofanyika kwa muda mrefu, kwani mara ya mwisho kikao kama hicho kilifanyika Septemba, 2017, Mhe. Hapi ametoa maelekezo kuwa kikao hicho kinatakiwa kufanyika mara mbili kwa mwaka.
Kufanyika kwa vikao hivyo kunafanya wafanyabiashara kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa na wajumbe wote, ili kufahamiana na kujadili mipango na mikakati, pia kuona changamoto na kuzijadili kwa pamoja, kwani ni muhimu Serikali kushirikiana na Sekta Binafsi. Changamoto zinazoikabili nchi yetu haziwezi kutatuliwa na Serikali peke yake, hivyo ni muhimu kuwepo na Sekta Binafsi, mfano shule, kilimo, ufugaji n.k. nini kifanyike kutatua changamoto hizi kama Mkoa.
Kuna madini katika Mkoa wetu ambayo yanapatikana sehemu mbalimbali kama Nyakavangala, Ifunda, Mlata lazima iendelezwe ili watu wafanye biashara za madini. Kuwekeza katika Sekta ya viwanda, maziwa, nguzo ili kuendeleza Mkoa wetu.
Pia kuendeleza vivutio kama Kalenga, Boma, mashamba ya chai ili watalii waingie kwa wingi katika Mkoa wetu. Mikakati mingi imewekwa kama kupanua kikwanja cha ndege,barabara ya kwenda Ruaha, kujenga mahotel ili watalii waupende Mkoa wetu.
Serikali imejipanga vizuri katika uwekezaji, ili kuwavutia watalii na wawekezaji katika kuwapatia ardhi, maji safi na salama, umeme na vyote vinapatikana bila shida na kwa wakati. Pia kuondoa kero zote kwa wawekezaji kama kunyanyaswa, kusumbuliwa, kuombwa rushwa, kutelekezwa na mengine mengi yanayofanana na hayo.
Nimetoa ombi kwa UNDP kwa ajili ya mambo haya:-
Pia alitoa agizo kwa TANESCO kuwa, kiwanda kikishawekwa mahali ni lazima umeme ufike hapo mara moja. TARURA nao walielekezwa kuhakikisha barabara zinaptika wakati wote wa mwaka, halikadhalika kwa Mamlaka ya Maji Safi na Salama. Pia Taasisi zote wanatakiwa kufahamu Mkoani kwake kuna wawekezaji wangapi/viwanda ili wajipange katika kutoa huduma husika.
Maendeleo ya Viwanda na Changamoto Zake
Taasisi kama Fire, Washer; msigeuke kuwa kero kwa wawekezaji, wanatakiwa kuelimishwa na kupewa ataraibu na sharia. Au kutoa onyo kama kunakuwa na makosa madogomadogo ambayo yanaweza kurekebishika.
Wakaguzi wanapokwenda kukagua viwanda ni lazima wapte kibali kwa Mkuu wa Wilaya husika, na waseme wanaenda kufanya nini. Hata kama ni Jeshi la Polisi wanaenda kumkamata muhalifu lazima Mkuu wa Wilaya ajue na atoe kibali. Ili kila anayetaka kuwekeza aione Iringa ni mahali salama.
Alimaliza kwa kusema kuwa, mkutano huu ni kwa ajili ya kujadili changamoto na mafanikio (maoni) karibuni sana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.