Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego amewataka Mafundi Mkoani humo kutumia Teknolojia ya Mawasiliano ili kutangaza kazi katika Mitandao.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua Kongamano la Fundi Smart lililofanyika katika Ukumbi wa Masit ambapo amesema kuwa ifike wakati sasa mafundi hao kuona umuhimu wa kutumia Teknolojua ya mawasiliano Vizuri ili kukuza na kutangaza kazi zao kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea kukua kwa uchumi mkoani hapo.
Pia Mhe. Dendego amewataka Mafundi hao kuachana na udanganyifu kwa wateja wao jambo ambalo linapelekea mafundi wengi kutokuaminiwa na Wateja wao na badala yake kupelekea hali ya uchumi kuwa Chini.
Aidha Mhe. Dendego Ameendelea kuwasisitiza Mafundi hao kuchangamkia mikopo inayotolewa na serikali itajayopelekea kukuza kazi zao.
Nae Mkurugenzi wa Fundi Smart Fredy Herbert amesema kuwa kutokana na Changamoto nyingi zinazowakumba Mafundi, kubwa ikiwemo mafundi hao kutapeliwa kwa sasa wamepata njia ya kuzuia changamoto hiyo kwa kuweka wanasheria ambao hao watakuwa watetezi wa Mafundi hao.
İmetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa İringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.