Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdory Mpango amewataka Watanzania kuachana na Mafundisho Potofu yakimiujiza Yanaoyotolewa na Baadhi ya Watumishi Nchini na Badala yake kuhakikisha wanafanya kazi kwa Bidii.Ameyasema hayo wakati wa Ibada Yubilei ya Miaka 125 ya Uinjilisti Jimbo la Iringa na Miaka 50 ya Ukuhani ya Mhashamu Ask. Tarcius Ngalekumtwa iliyofanyika kwenye viwanja vya kichangani katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Mhe. Mpango Amesema Kuwa Katika Zama Hizi za Uinjiilishaji Kumekuwa na Changamoto Kubwa ya Kuenea kwa Mafundisho Potofu na Imani Kali za Kidini jambo ambalo limepekea watu wengi kutokufanya kazi na kukimbila kwenye miujiza ambayo miujiza hiyi imekuwa ikiwanufaisha na kuwatajirisha watu.Aidha Mhe. Dkt Mpango ameendea kwa kusema kuwa mbali na hayo kuendelea kutokea katika jamii hii lakini bado wapo baadhi ya Wahubiri wamekuwa Wakishabikia Baadhi ya Matendo maovu ikiwemo masuala ya ushoga jambo ambalo linaleta mmong’onyoko wa Maadili.Akitoa Taarifa ya Mkoa Mhe. Halima O. Dendego (Mkuu wa Mkoa wa Iringa) amesema kuwa katika Mkoa wa Iringa kumeendelea kuwa na Amani na Usalama kwani Dini na Serikali vimekuwa vikishirikiana vizuri katika kuhakikisha wanalinda Amani na kukuza maendeleo katika Mkoa .Pia Mhe. Dendego Ameendelea kutoa shukrani kwa taasisi za kidini kwani zimeleta Maendeleo makubwa katika Jamii kwa kufungua shule , hospitali na vitu vingi vinavyomuwezesha mtu kuweza kujikwamua kiuchumi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.