Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Iringa
Kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa imehakikishiwa kufanya kazi kwa amani na usalama mkoani Iringa kutokana na vyombo vya usalama kuwa macho muda wote.
Uhakika huo ulitolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiongea na kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kamati hiyo ilipofanya ziara mkoani hapa.
Masenza ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa Mkoa wa Iringa upo shwari. Hali ya usalama ni nzuri kuiwezesha kamati hiyo kufanya ziara ya kikazi katika hali ya usalama na utulivu. Aidha, aliongeza kuwa wananchi mkoani Iringa wanajitambua katika kutekeleza majukumu yao. “Wananchi mkoani Iringa hasa wakulima katika msimu huu wa kilimo wanajitambua na hawashurutishwi kutekeleza majukumu yao ya kilimo” alisema Masenza.
Wakati huohuo, makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa, Mwanne Mchemba alisema kuwa dhumuni la ziara ya kamati yake ni kukagua miradi ya maendeleo wilayani Kilolo kwa fedha zilizotolewa na serikali mwaka 2016/2017. “Tunajua kuwa mkuu wa Mkoa ni jembe katika usimamizi wa uhamasishajai wa maendeleo. Hivyo, kamati inataka kujiridhisha na matumizi ya fedha za serikalai hasa thamani ya fedha kabla ya serikali kuidhinisha fedha nyingine kwa Wilaya ya Kilolo” alisema Mchemba.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.