“ Hakika mashindano haya ya UMITASHUMTA na UMISSETA yamekuwa faida kubwa kwani yamechagiza Uchumi wa Mkoa wetu na kutangaza vivutio vya Utalii vya Mkoa wa Iringa Kitaifa, kwani Mashindano yamepokea washiriki 10000 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Kheri James alipokuwa akitoa salamu za Mkoa kwenye ufungaji wa Mashindano ya UMISSETA yaliyohitimishwa na Mheshimiwa Festo Dugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mkoa wa Iringa.
Kheri James kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Iringa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuichagua Iringa kuwa waandaaji wa Mashindano ambayo yatafanyika kwa miaka mitatu mfululizo.
Mashindano ya UMISSETA yalifunguliwa rasmi Juni 20,2025 na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwijuma na yanaandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yalifunguliwa rasmi tarehe 8/6/2025 na yamehitimishwa leo tarehe 29/6/2025 na Mheshimiwa Festo Dugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mkoani Iringa.
Washindi katika Mashindano haya wamekabidhiwa makombe na nishani mbalimbali.
#ortamisemi #tanzania
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.