Leo tarehe 3/2/2023 Mhe. Halima Omary Dendego Mkuu wa Mkoa wa Iringa amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa, katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Masiti uliopo kata ya gangilonga.
Na baadae Mhe. Dendego alipata wasaa wa kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita yanayotekelezwa Mkoani Iringa.
Mhe. Dendego ametumia fursa hii kuelezea watanzania na wana iringa ili wajue tunaposema Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa anaupiga mwingi ndio wajue maana ametuletea fedha nyingi sana Mkoa wa Iringa ambazo tumetekeleza miradi mingi kupitia sekta zilizopo ndani ya Mkoa.
" Wastani wa pato la Mkoa limefikia shilingi trilioni 4.630 kutoka shilingi trilioni 3.584 mwaka 2015".
Akitoa salamu za chama cha mapinduzi Comred Daud Yassin Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Iringa amepongeza sana Mhe. Dendego Mkuu wa Mkoa Iringa kwa kuandaa kongomano hili zuri na kutangaza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwani amewasaidia kwa CCM kuelezea mafanikio yalipo katika Ilani ya CCM nao watatumia nakala ya hiyo kuisambaza kweye ofisi zote za chama ili iwe dira nzuri ya kuwaeleza wananchi wajue mambo mazuri na makubwa yanayofanywa na serikali ya Mkoa Iringa.
Mhe. Halima Dendego Mkuu wa Mkoa Iringa aliwashukuru wajumbe wote walioshiriki kongamano hilo na kuwatakia safari njema na majukumu mema ya ujenzi wa Taifa.
Imetolewa na Afisa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.