Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga, amesema anatarajia kufanya kazi na wananchi wa Iringa ili kuendeleza mambo yote ya kiuchumi na kukaa na kamati zote pamoja na wafanyabiashara katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana
Hayo ameyasema leo tarehe 24.05.2021 katika ukumbi wa Siasa na Kilimo akikabidhiwa rasmi Ofisi ya Mkoa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally Hapi ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Pia Mhe. Queen ameahidi kusimamia haki na kushughurikia changamoto zote za wananchi wa Iringa ikiwa ni pamoja na kusimamia llani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo amekabidhiwa na uongozi Wa Chama asubuhi ya Leo katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa
"Naahidi kufanya kazi na ilani ya chama ambayo nimekabidhiwa leo asubuhi na uongozi Wa chama ili kutekeleza yale yaliyoelekezwa ndani ya Ilani katika
kuleta maendeleo,"alisema Mhe. Queen
Hata hivyo alisema atasimamia na kuendeleza kaulimbiu ya 'Iringa Mpya' ambayo iliazishwa na kiongozi wa zamani huku akichanganya na yake inayosema uwajibikaji rafiki wa maendeleo
Naye, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Zamani mkoani hapa, Ally Happy, amesema anaondoka Iringa huku akiwa bado anawapenda wananchi wa mkoa huo kutokana na uchapakazi wao , ushirikiano, pamoja na moyo wa kujitolea waliokuwa nao
Alisema yawezekana aliwakwanza baadhi ya watu kutokana na kusimamia haki katika utendaji wake hivyo Kama kunamtu alimkwanza katika majukumu yake amsamehe
"Naondoka nikiwa bado nawapenda kwa yeyote niliyomkwanza anisamehe nilijitoa kwaajiri ya wanaIringa ila ninaimani na huyu kiongozi nawahakikishie kwamba linaondoka jembe linakuja jembe,"alisema.
Aidha amesema katika uongozi wake alisimamia haki alitatua migogoro alitembelea kila Kijiji anasema yote hayo alifanya kwaajiri ya wanaIringa
Hivyo amewaomba wakazi wa Iringa wasimtenge kiongozi wao mpya wasirudi nyuma wala kumkatisha tamaa bali waoneshe ushirikiano katika ngazi zote
"Nikuahidi Kiongozi wakazi wa Iringa ni wachapakazi ,wanajituma ,wanamoyo wa kujitolea wanalima wanachangia miradi wakikupenda wamekupenda hawana moyo wa unafiki, alisema Happy
Omary Nzowa, ambaye ni mkuu wa baraza la wazee Mkoani hapo, alisema atamkumbuka kiongozi huyo kutokana na utendaji wake wa kazi lakini hana budi kumuaga na kumkalibisha kiongozi mpya na wateendelea kumuombea pamoja na kumpa ushirikiano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.