Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewaasa Viongozi na watumishi Mkoa wa Iringa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidi ili kuleta maendeleo ndani ya Mkoa na taifa kwa ujumla
Mhe. serukamba amebainisha hayo Mei, 07,2025 wakati wa kikao cha utekelezaji wa miradi kilichowakutanisha wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na wataalamu kutoka katika Halmashauri kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa ambapo amesema kuwa ili Mkoa uweze kuwa na maendeleo ni lazima wakurugenzi na wataalamu waliopo kwenye Halmashauri waweze kuwajibika ipasavyo kuhakikisha wao wanakuwa wa kwanza katika kumsaidia Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
"sisi oste tumekutana hapa ni kwasababu ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye aliyetukutanisha hivyo tupo hapa tufanye kazi kwa bidii tuweze kuwahudumia wananchi na kutekeleza yale yote ambayo tumeagizwa kuyafanya hivyo niwaombe ndugu zangu na kuwasisitiza uwajibikaji katika kazi zenu"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.