Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda, leo ametoa pongezi kwa Maafisa elimu wa wote walipo ndani ya Mkoa kwa juhudi mbalimbali walizozifanya ambazo zimeongeza ufaulu ndani ya Mkoa.
Pongezi hizo zimekuja wakati mkoa wa Iringa ukishika nafasi ya tatu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2021.
“Hongereni sana nyote kila mmoja kwa nafasi yake. Vile vile pongezi za dhati kwa kuongeza ufaulu bora kwa mtihani wa ki Taifa wa kidato cha nne kutoka 40.5% mwaka 2020 mpaka 41.1% mwaka 2021 sawa na ongezeko la 0.6%.”
Pia amewataka Maafisa elimu hao toka Halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa weredi, kanuni, taratibu na sheria katika kuongeza juhudi ili kuhakikisha Mkoa wa Iringa unashika nafasi ya kwanza (1) ki Taifa.
Bi, Happynes Seneda (RAS) ametumia kikao hicho kuwakumbusha Maafisa elimu hao kuwatendea haki watumishi waliochini yao, pamoja kuwa na majibu mazuri kwa watumishi na kutatua kero zao, " wapo baadhi ya Maafisa hapa wana majibu mabaya sana kwa watumishi na hii inapelekea baadhi ya watumishi kuja kuleta malalamiko Mkoani acheni hiyo tabia hizi nafasi mpewa kwa neema ya MUNGU tu hivyo watendeeni haki wenzenu".
Katika kikao hicho Kaimu Afisa Elimu Mkoa bi, Mwasumile amemshukuru Ras na amemwaidi kuwa wamejipanga vizuri na wanaamini watashika nafasi ya kwanza Ki Taifa.
Imetolewa na Afisa habari na uhusiano Mkoa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.