Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Serikali inawaheshimu wafanyakazi kwa sababu ndiyo njia ya kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo ilitolewa na waziri wa nchi Ofisi nya Waziri mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama alipofika kusaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa mkoa leo asubuhi.
Waziri Mhagama alisema kuwa serikali inawaheshimu wafanyakazi wa sekta zote nchini kutokana na nafasi yao katika ujenzi na ukuzaji wa uchumi. Alisema kuwa katika utekelezaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda, wafanyakazi ni njia muhimu katika utekelezaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda nchini. Alisema katika maadhimisho ya seherehe za Mei Mosi, limeandaliwa kongamano la Tanzania ya viwanda kwa lengo la kufafanua dhamira ya serikali kuelekea uchumi wa viwanda.
Aidha, alimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza kwa kukubali kubeba jukumu la kuwa mwenyeji wa sherehe za Mei Mosi kitaifa mwaka huu. Alielezea imani yake kwa uongozi wa mkoa katika kufanikisha sherehe hizo mkoani hapa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa, alisema kuwa wananchi wa Iringa wapo tayari kuwapokea wageni na kusherehekea pamoja nao. Alisema kuwa maandalizi yanaenda vizuri yakitanguliwa na michezo mbalimbali na makongamano.
Sherehe za Mei Mosi kitaifa mwaka 2018 zitafanyika mkoani Iringa na mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.