Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Eng. Leonald Masanja amezitaka Halmashauri na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Kuweka Miakakati na Malengo kuhakikisha inaongeza vituo vya kutolea huduma za dharula na upasuaji ili kupunguza Vifo Vitokanavyo na uzazi na Watoto Wachanga.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, wakati Ufunguzi wa Kikao cha kanda ya Nyanda za juu Kusini kilichofanyika leo tarehe 14/09/2023 katika chuo kikuu kishiriki Mkwawa kilichopo Mkoa wa Iringa Ndugu Masanja amesema kuwa mikoa ya Nyanda za Juu kusini kuna upungufu wa vituo vinavyotoa huduma ya dharula na upasuaji hivyo ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na Watoto Mikoa na Halmashauri na iweke malengo makubwa katika kuongeza vituo hivyo
Pia Ndugu Msanja amesema kuwa kupitia kikao hicho Serikali itaendelea kuhakikisha inapunguza vifo vitokanavyo na uzazi na Watoto kwa kuwawezesha watoa huduma kuwapa uwezo na kuwatia moyo katika kazi zao.
Nae mwakilishi wa Mama na Mtoto kutoka TAMISEMI Mary Shadrack amesema kuwa wao kama ofisi ya Rais TAMISEMI wameendelea kuboresha Vituo vya afya kwenye Mikoa yote nchini lakini wameendelea kujenga vituo vingine vya afya ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi mahali walipo. aidha ameongeza kwa kusema kuwa sambamba na hayo pia wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa ajira za wahudumu katika sekta ya afya kwani kwa ongezeko hilo linapelekea kupunguza matatizo mbalimbali katika jamii.
Kikao hicho kimewakutanisha watumishi toka mikoa mitatu ikiwemo Iringa, Njombe na Ruvuma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.