Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, IRINGA
Serikali mkoani Iringa imewataka wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Nyakavangala wilayani Iringa kujihadhari ya maambukizi ya virus vya Ukimwi mgodini hapo.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakavanga wilayani Iringa leo.
Masenza alisema kuwa maambukizi ya virus vya Ukimwi katika Mkoa wa Iringa yapo kwa kiwango cha juu. Aliwataka wachimbaji wadogo katika mgodi wa Nyakavangala kujitunza ili kutokupata maambukizi hayo. Alisema asilimia kubwa ya wachimbaji ni vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa. Iwapo nguvu kazi hiyo itaugua ugonjwa wa Ukimwi familia zao zitapoteza nguvu kazi na Taifa pia. Vilevile, aliwakumbusha kuwa kipindupindu bado ni changamoto katika baadhi ya maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.