• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

WADAU WA VVU/UKIMWI IRINGA WATAKIWA KUJITATHMINI

Posted on: December 16th, 2017

Na Ofisi ya mkuu wa Mkoa

Wadau wa mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU na Ukimwi wametakiwa kujitathmini katika utekelezaji wa mkakati wa kupambana na VVU baada ya mbinu za awali kuonesha kushindwa.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akifungua kikao cha kuutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kilichofanyika katika hoteli ya Gentle Hills iliyopo mjini Iringa.

Ayubu alisema matokeo ya utafiti wa VVU na UKIMWI (2016/2017) yameonesha kuwa maambukizi ya VVU mkoani Iringa yameongezeka kutoka asilimia 9.1 hadi 11.3. “Maambukizi ya VVU mkoani Iringa yameongezeka kutoka asilimia 9.1 ya awali (2011/12) kufikia asilimia 11.3 (2016/17). Hii ni ishara wazi kuwa maambukizi mapya yameongezeka kwa asilimia 2.2” alisema Ayubu.

Aidha, aliwataka wadau wa mapambano dhidi ya VVU kujitathmini ili kuona maeneo ambayo hawakufanya vizuri. “Tunatakiwa tujitathmini kuona ni wapi ambapo hatujafanya vizuri katika utekelezaji wa program zetu za mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU” alisema Ayubu.

Katibu Tawala Mkoa alisema kuwa wadau wa maendeleo wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika kuwaletea maendeleo na kuboresha afya za wananchi mkoani Iringa. “Uwepo wenu katika Mkoa huu umeongeza kasi ya serikali ya Mkoa na Halmashauri zake ya kuwafikia wananchi katika jitihada zao mbalimbali za kukabiliana na changamoto za maisha, hasa kujikwamua kiuchumi na kuimarisha afya zao” alisema Ayubu.

=30=




Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • KUELEKEA MBIO ZA THE GREAT RUAHA MARATHON

    July 01, 2025
  • MAAFISA ELIMU WAAGIZWA KUSIMAMIA MAENDELEO YA MICHEZO MASHULENI

    June 29, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 YACHAGIZA UCHUMI WA IRINGA.

    June 29, 2025
  • KARIBU MKOANI IRINGA

    June 28, 2025
  • View All

Video

MAENDELEO KWA SASA BILA MAWASILIANO HAYAWEZEKANI- RC KHERI
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.