Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wameelewa dhana serikali ya awamu ya tano ya utoaji wa elimu bila malipo na kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi, Allan Benard alipokuwa akisoma risala ya utii ya wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa mkesha wa Mwenge wa uhuru katika Kata ya Igowole, Tarafa ya Kasanga wilayani Mufindi.
Benard alisema kuwa wananchi wameelewa vizuri dhana ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt John Magufuli ya elimu bila malipo nchini. “Hii inadhihirishwa na ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa kila mwaka, kupungua kwa utoro katika shule za msingi na sekondari, ambapo mahudhurio ya wanafunzi yameongezeka kwa shule za msingi kwa asilimia 96 (2015), asilimia 98 (2018) na sekondari ni asilimia 80 (2015) hadi asilimia 88 (2018)” alisema Benard. Wananchi kushiriki katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ni ishara ya uelewa wa dhana hiyo. “Jumla ya daharia 22 zimejengwa katika shule za sekondari kwa ushirikiano wa wananchi na halmashauri. Pia wananchi kuchangia chakula cha wanafunzi. jumla ya shule 72 za msingi kati ya 147 zinatoa chakula cha mchana na shule 26 za sekondari kati ya shule 33 zinatoa chakula kwa wanafunzi” aliongeza Benard.
Ikumbukwe kuwa tangu kuanza kwa mpango wa elimu bila malipo nchini mwezi Disemba, 2015 hadi mwezi Machi, 2018 halmashauri imepokea jumla ya shilingi 3,015,122,456 kwa ajili ya fidia ya ada, fedha ya chakula kwa wanafunzi wa bweni na ruzuku ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule za sekondari.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.