Wananchi wa kata ya Mpanga Tazara Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi mkubwa wa ujenzi wa shule ya Sekondari.
Wananchi hao wametoa shukurani zao walipojitokeza katika zoezi la ujenzi wa shule hiyo lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Halima Dendego ambapo wamesema wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi mkubwa katika kata hiyo, mradi ambao unakwenda kutimiza ndoto za watoto wao kwenda shule.
Pia wamesema kuwa uwepo wa shule hiyo, licha ya kupunguza adha ya watoto kutembea umbali wa zaidi ya Km 30, kwenda katika shule ya sekondari Mgololo itasaidia watoto wengi wa eneo hilo kupata Elimu kama ilivyo haki ya mtoto wa kitanzania.
"tumefuhi sana kujengewa shule hapa kijijini, watoto wetu waliteseka kwenda umbali mrefu, hata sisi wazazi hatukuwa na amani pale watoto walipokwenda shuleni mbali hasa kipindi cha mvua, kwa ukaribu huu wa shule, tutakuwa na amani na watoto watafurahi,na pia kutakuwa na mahusiano mazuri kati ya mzazi na mwalimu maana inakuwa shida sana siku mzazi unapohitajika shuleni unakuta gari moshi hiyo siku halipiti hivyo unasubiri mpaka pale gari moshi litakapopita kwa kweli tunamshukuru Mama Samia " Amesema Gift Kivaya
Akizungumza na wananchi hao Mhe. Dendego amewataka wananchi hao kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani bado itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika kata hiyo.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo Mkuu wa shule ya Sekondari Mdabulo Mwalimu Jumanne Nyaulingo amesema kuwa wamepokea Zaidi ya shilingi milioni mia tano themanii na tatu kwaajili ya ujenzi na kusema kuwa changamoto kubwa waliokumbana nayo ni usafirishaji wa vifaa vya ujenzi na hii imesababishwa na miundombinu ya barabara kutokuwa rafiki kwa usafirishaji wa vifaa hivyo.
Mhe. Dendego amekuwa na ziara ya siku saba ambapo kwa siku tatu amekuweka kambi katika kata ya Mpanga Tazara na Kulala katika Shule ya Msingi ya Mpanga Tazara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.