Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amewataka watunza kumbukumbu nchini kuhakikisha wanakuwa na uaminifu na watunza siri katika utendaji wao wa kazi.
Ameyasema hayo leo Mei, 07, 2024 wakati alipo muwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwenye ufunguzi wa kikao kazi na mafunzo maalumu kwa watunza kumbukumbu kutoka Tanzania bara na visiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Masit Mjini Iringa.
Akizungumza na watendaji hao Mhe. James amesema kuwa moja ya kazi ya kuiheshimu ni kazi ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka hivyo suala la uadilifu,uaminifu na utunzaji wa siri unapaswa kupewa kipaumbele katika utendaji wa kila siku wa shughuli za Serikali.
Akitoa taarifa kwa Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TRAMPA Ndg. Devota Mlope amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuweza kuwajengea uwezo watunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika utendaji wa shughuli zao za kila siku ambapo mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uhodari na kuongeza tija na ufanisi.
Nao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi pindi wawapo Ofisini huku wakiiomba Serikali kwenye mafunzo hayo kuungana na viongozi wa ofisi kuwajengea uwezo ili nao wapate Elimu ya utunzaji wa siri kwani wao wamekuwa wakitunza siri kutokana na Taaluma yao lakini viongozi walio juu baadhi yao wamekuwa sio waaminifu.
Zaidi ya watunza kumbukumbu Elfu moja kutoka Tanzania Bara na Visiwani wameudhuria mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa siku nne.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.