• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), DANIEL CHONGOLO AMEITAKA SERIKALI KUHARAKISHA MCHAKATO WA MABADILIKO YA MITAALA YA ELIMU

Posted on: May 28th, 2023

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameitaka serikali kuharakisha mchakato wa mabadiliko ya mitaala ya elimu itakayowawesha wahitimu wake wa ngazi mbalimbali kuwa na taaluma ya kujitegeme badala ya kuajiriwa. “Tunataka mitaala itakayowajengea uwezo vijana na wahitimu wetu kwa ujumla kujiajiri kuliko kutegemea kuajiriwa,” Chongolo ameyasena hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Malangali, wilayani Mufindi.

Chongolo alisema mazingira ya sasa ya elimu nchini imewafanya baadhi ya wahitimu wakiwemo wa vyuo vikuu kuwa wategemezi badala ya wabobezi. “Kama ni kilimo, biashara, uhandisi, udaktari na fani nyingine yoyote, tuwe na mitaala itakayoanza kuwaandaa vijana wetu toka ngazi ya chini kabisa kuwa wabobezi katika fani hizo,” alisema msimamo wa CCM ni kuwa na mitaala hiyo mipya na Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekwishatoa kibali kwa Wizara ya Elimu kuja na mitaala hiyo haraka. “Zamani katika shule zetu nyingi kilimo lilikuwa somo la lazima toka ngazi ya chini. Tuliopata bahati ya kusoma wakati wa mfumo huo tulijengewa msingi wa kuwa wajasiriamali hata kama hakuna ajira,” alisema. 

Awali Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi, Dk Sophia Mjema aliitaka jamii kuwekeza nguvu kubwa itakayomuwezesha mtoto wa kike kufikia ndoto za elimu. Pamoja na kuhakikisha maadili ya mtanzania na watoto wanalindwa pamoja na kupewa haki zao zote, Dk Mjema alisema watoto wa kike wakiendelezwa wanayo fursa ya kuwa viongozi wakuu kama ilivyo kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan na kujiimarisha kiuchumi.

Katika mkutano wake huo wa siku ya pili ya ziara yake mkoani Iringa, Chongolo aliyeambatana pia na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Ussi (Gavu) alipokea taarifa, kero na maombi mbalimbali toka kwa wadau wa kata ya Malangali na kuzipatia ufumbuzi.

Amechangia Sh Milioni nne kati ya Sh Milioni 9.7 kukamilisha ujenzi  wa msikiti wa Malangali huku Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini David Kihenzile akichangia Sh Milioni tatu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Leonard Mahenda akichangia Sh Milioni mbili na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego  Sh 700,000.

Aidha amejibu ombi la Kihenzile kuhusu barabara ya Mbalamaziwa Malangali linalotaka ijengwe kwa kiwango cha changarawe akimtaka Mkuu wa Mkoa kufuatilia taarifa za ujenzi huo na kuzifikisha kwake ili azifanyie kazi.

Chongolo ameahidi pia kukitafutia kituo cha afya Malangali gari la wagonjwa pamoja na mashine ya mionzi (X ray)- aliyoahidi kuileta mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi kujenga chumba kwa ajili ya huduma hiyo.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliwambia wananchi wa kata hiyo kwamba serikali imetoa zaidi ya Sh Milioni 600 kwa shule ya sekondari Malangali kwa ajili ya ukarabati wa hosteli za wanafunzi.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.