Halmashauri ya wilaya ya Kilolo imejipanga kuongeza fedha kwa ajili ya maandalizi ya Nanenane ili kuhamasisha matumizi ya teknolojia kwa lengo la kuonesha matumizi ya teknolojia katika kilimo na ufugaji.
Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, Vallence Kihwaga alipoongea na wanahabari katika ziara yake ya kukagua banda la maonesho la Halmashauri ya wilaya ya Kilolo jana mjini Mbeya.
Kihwaga alisema “Halmashauri yangu imedhamilia msimu ujao wa Nanenane kuanza maandalizi mapema na kuongeza fedha ili maonesho katika banda letu yawe bora zaidi”. Aliongeza kuwa maandalizi yatakapoanza mapema yataiwezesha Halmashauri kukusanya wadau wengi wa kuonesha teknolojia bora za kilimo na ufugaji.
Akiongelea tofauti ya naonesho ya mwaka jana na mwaka huu, mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo alisema kuwa Halmashauri yake imeongeza matumizi ya teknolojia katika kilimo. Aliitaja teknolojia hiyo kuwa ni uanzishwaji teknolojia ya “green house” na matumizi ya chokaa mazao.
Maonesho ya shughuli za wakulima Nanenane mwaka 2017 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kufikia uchumi wa kati”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.