Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishahi Mkoa wa Iringa Ndug. Elias Luvanda akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa ametoa wito Kwa Wananchi wa Mkoa wa Iringa kujitoleza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria wa Mama Samia Utakao zinduliwa Disemba 10, 2024 katika Viwanja vya Mwembe Togwa.
Ameyasema hayo leo Disemba 09, 2024 Wakati akizungumza na Wanahabari pamoja na wataalamu mbalimbali wakiwemo Maafisa Ardhi, Wanasheria, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Dawati la Jinsia Polisi, Wasaidizi wa Kisheria, pamoja na Mawakili wa kujitegemea.
Hata hivyo Kampeni hii itahusisha utoaji elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria ikiwemo Maswala ya Ardhi, Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mirathi, Ndoa, Ukatili wa Kijinsia, Madai, Jinai vilevile itahusisha huduma ya usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa na kifo vitakavyotolewa na RITA.
Aidha Kampeni ya Msaada wa kisheria wa Mama Samia unategemea kufanyika Mkoani Iringa ndani ya Siku kumi kwa lengo la kuwasaidia Wananchi wenye changamoto za kisheria Bure.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.