Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) chini ya mwenyekiti wake Mhe. Halima Mdee imeielekeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuimarisha usimamizi na kufanya ufatiliaji wa miradi yote inayotekelezwa katika Mkoa.
Maelekezo hayo yametolewa katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri za Mkoa wa Iringa.
Mhe. Dr Hamis Kigwangalla mjumbe wa kamati hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa LAAC, Halima Mdee.
"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iimarishe usimamizi na kufanya ufatiliaji wa mara Kwa mara kwa miradi yote inayotekelezwa katika Halmashauri zote za Mkoa Iringa".
Amesema, usimamizi huu ufanyike katika hatua zote za utekelezaji wa miradi ili kubaini dosari zinazoweza kuondoa thamani ya fedha na kuchukua hatua stahiki.
Naye, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa serikali kupitia TAMISEMI itafanyia kazi mapungufu yote yaliyoainishwa na Kamati ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika kwa manufaa ya wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.