• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

MAAFISA MAENDELEO WATAKIWA KUHAMASISHA UJENZI WA VYOO IRINGA

Posted on: December 3rd, 2017


Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Maafisa maendeleo ya jamii wa halmashauri watakiwa kushiriki katika kuhamasisha kampeni ya ujenzi wa vyoo ili kuwa na jamii yenye vyoo bora na isiyokuwa na magonjwa ya mlipuko.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya kukagua hali ya ujenzi wa vyoo katika halmashauri ya wilaya ya Iringa jana.

Masenza alisema “kasi ya ujenzi wa vyoo bora si ya kuridhisha. Kuna haja ya kufanya tathimini ya kampeni ya ujenzi wa vyoo katika mkoa wa Iringa ili tuone jinsi ya kujipanga zaidi na kubadilisha mkakati. Lazima ufike wakati tusema katika Mkoa wa Iringa kutokuwa na choo bora mwisho”. Aliongeza kuwa maafisa maendeleo ya jamii hawajatumika ipasavyo katika kampeni ya ujenzi wa vyoo. Aliziagiza mamlaka za serikali za mitaa kuwatumia maafisa hao ili wasaidie uhamasishaji jamii katika ujenzi wa vyoo bora kwa wananchi. Aidha, aliwataka watendaji wa Kata na Vijiji kutekeleza wajibu wao katika kusimamia ujenzi wa vyoo katika maeneo yao ili zoezi hilo likamilike mapema.

Wakati huohuo, kaimu afisa mazingira katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa, Hawa Mwechaga alisema kuwa baadhi ya vyoo vinavyojengwa ni vidogo kiasi cha kutosha kuwahifadhi watu wembamba pekee. Alishauri kuwa wananchi waelimishwe na kusimamiwa ili wajenge vyoo vyenye nafasi ya kutosha kuweza kuwahifadhi hata watu wanene. Alisema kuwa choo ni muhimu kiwe na nafasi kwa sababu kinamsitiri na kumuhifadhi mtumiaji wake.

Mkuu wa mkoa wa Iringa alifanya ziara ya kukagua hali ya usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo katika kata za Isakalilo, Mseke na Mgama katika halmashauri ya wilaya ya Iringa

=30=










Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ‎RC SERUKAMBA AITAKA TRA KUDHIBITI RISITI FEKI, KUHAMASISHA ELIMU YA KODI

    May 19, 2025
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA WA IRINGA.

    May 18, 2025
  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.