Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameongoza mbio za Great Ruaha Marathon zilizofanyika mkoani Iringa katika hifadhi ya Taifa ya Wanyamapori Ruaha.
Majaliwa ameshiriki mbio za Great Ruaha Marathon Julai 06, 2024 ambapo mbio hizo zilijumuisha washiriki wengine waliokimbia umbali kuanzia Kilomita 5, 10, 21 na 42.
Miongoni mwa viongozi wengine walioshiriki mbio hizo ni pamoja na manaibu waziri ambao pia ni wabunge wa kutoka majimbo tofauti tofauti mkoani Iringa, viongozi wa Serikali na Viongozi wa vyama vya siasa.
Mbio hizo zinalenga kukuza utalii wa Kusini na kutoa hamasa kwa jamii kuhifadhi mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji vya Mto Ruaha mkuu.
Pia Mbio hizo zinaunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha na kukuza sekta ya Utalii nchini.
Pamoja na lengo kuu la kuhamasisha Utalii na utunzaji wa vyanzo vya maji mto Ruaha mkuu Waziri Mkuu amehamasiaha kuhamasisha mazoezi na afya bora.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.