Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa amefanya uzinduzi wa kikao cha kupokea maagizo ya Miongozo Mitatu ya Kuboresha Elimu ya Misingi na Sekondari uliotolewa Agosti mwaka huu Mkoani Tabora na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa katika uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Shule ya wasichana Iringa.(Iringa gilrs) Katika uzinduzi huo Mhe Halima Dendego amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya huku akiwaahidi kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha walimu wanapatiwa haki zao za msingi na wanawajibika katika kutoa Elimu Bora. Aidha Mhe. Halima Dendego amesema “Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kila mwaka tutakuwa tunaandaa kikao cha tathimini kwa sekta ya Elimu ili tuweza kuona mafanikio,changamoto na mambo yanayofuata siku za mbele tuweza kuyakabiliwa kwa Pamoja”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.