• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

MKUU WA MKOA IRINGA AWATAKA WADAU WOTE KUSHIRIKI UJENZI WA VIWANDA 100

Posted on: February 1st, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Iringa

Wadau wa maendeleo mkoani Iringa wametakiwa kushirikiana katika utekelezaji wa lengo la uanzishaji wa viwanda 100 ili kukuza uchumi wa wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua kikao cha mrejesho wa kampeni ya “Mkoa wetu, viwanda vyetu” pamoja na maandalizi ya maonesho ya utalii karibu kusini kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo jana.

Masenza alisema “katika kutekeleza azma hii ya serikali ya uchumi wa viwanda, tumepewa mwaka mmoja kuhakikisha Mkoa wetu unaanzisha viwanda si chini ya viwanda 100. Hayo ni malengo, lakini utekelezaji wake unategemea sana wadau wote kwa pamoja tunavyoshirikiana kukamilisha agizo hili la serikali”.  Aidha, aliwataka wadau wote kutumia fursa hiyo ya uanzishaji viwanda kujikomboa kiuchumi na wananchi kwa ujumla wake.

Katika utekelezaji wa lengo hilo, alisema taasisi nyingine zimewekewa malengo ya utekelezaji. Alizitaja taasisi hizo kuwa ni SIDO Mkoa wa Iringa kujenga viwanda visivyopungua 20. Aliongeza kuwa taasisi kama madhahebu ya dini na vyama vya ushirika pia vimeonesha nia ya kujenga viwanda mkoani Iringa.

Kikao cha kupokea mrejesho wa kampeni ya Mkoa wetu viwanda vyetu kililenga kupokea utekelezaji kwa kuonesha mafanikio na changamoto katika utekelezaji huo.

=30=

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ‎RC SERUKAMBA AITAKA TRA KUDHIBITI RISITI FEKI, KUHAMASISHA ELIMU YA KODI

    May 19, 2025
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA WA IRINGA.

    May 18, 2025
  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.