Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga amepokea ugeni ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa
Imekuwa siku njema ambayo inaleta mwanga mwingine wa siasa nchini Tanzania.
Lengo la ugeni huu mbali ya kusalimia ilikuwa ni kuhusu masuala ya amani, mshikamano, umoja wa Tanzania na kuweza kufanya siasa zenye faida kwa Watanzania,
Nimeahidiana na Mh Mbowe kufanya siasa njema kwa kila mmoja kwa upande wake na kuheshimiana.
Masuala ya mkoa yanatatuliwa na wanamkoa, sio kwenye mtandao. Mkoa wa Iringa tutaanza kuitenda hiyo amani kwa vitendo kama ambayo mmeona amani na utulivu ndio ambalo Rais Samia analitazama.
Karibu tena Iringa Mh Mwenyekiti Mbowe
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.