Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego ameipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kupata Hati Safi kwa Hesabu zinazoishia tarehe 30 Juni, 2022.
Akiwa kwenye kikao Cha Baraza maalumu la madiwa la kujibu hoja za CAG mhe, Dendego amewataka waheshimiwa maadiwani Halmashauri ya Mji Mafinga kuifahamu vizuri miradi inayotekelezwa kwenye Kata zao Kwa sababu wao ndio jicho la karibu la Mkuu wa mkoa, pia inatakiwa kujua miradi na muda wa
Utekelezaji wa mradi Ili kujua thamani ya fedha iliyotumika kama inaendana na mradi unaotekelezwa kwenye kata yake
Mheshimiwa Dendego ameitaka Halmashauri ya Mji Mafinga kuhakikisha wanatumia mafundi wenye sifa katika kutekeleza miradi inayotekelezwa kwa kutumia force account Ili kuondoa hoja zisizo na tija.
Ndugu Eng, Leornad Massanja Katibu Tawala Mkoa wa iringa amesema kuwa Kuna hoja zingine ni nyepesi zinaweza kufungwa mapema kama menejimenti ya halmashauri itazijibu vizuri pasipo kuleta hadithi.
Eng, Massanja amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa mafinga kumletea orodha ya watumishi wote wanaotuhimiwa kuanziaha vikundi hewa na kuchukua mkopo wa halmashauri hiyo na kusababisha hoja Kwa mkaguzi wa nje (CAG) kupitia kikundi kinachoitwa mnyigumba " naagiza ndani ya siku 3 nipate orodha hiyo Ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wahusika wote kuanzia mwenyekiti, katibu na mwekahazina wa kikundi hicho".
Baadae Mhe. Halima Dendego aliagiza waitwe maafisa watendaji wa kata na Maendeleo ya jamii wote, akiwa kwenye kikao hicho cha pili na maafisa hao ametoa wiki 2 kuanzia Leo hii Kila afisa ahakikishe anaenda kukusanya fedha hizo za mkopo wa halmashauri Kwa sababu wanavijua vikundi vizuri na wala ataki kusikia habari kwamba vilivunjika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Amefikia hatua hiyo Mhe Dendego baada ya kuona Kwa asilimia kubwa za hoja zinausisha vikundi vilivyochukua mikopo kwenye halmashauri hiyo na hakuna urejeshwaji Kwa kisingizio baadhi ya vikundi vimesambalatika.
Imetolewa na Afisa habari ofisi ya Mkuu wa mkoa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.