• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

RC MASENZA ASHAURI MATUMIZI YA TEHAMA MAHAKAMA KUU IRINGA

Posted on: January 30th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza ameishauri Mahakama kuu kanda ya Iringa kuongeza kasi ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa haki kwa wananchi.

Kauli hiyo aliitoa katika salamu zake kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria nchini uliofanyika katika uwanja wa Mahakama kuu Iringa jana.

Masenza alisema kuwa faida za Tehama katika Mahakama ni kurahisisha utoaji haki kwa wakati kwa wananchi. Aliongeza kuwa Tehama inasaidia kutunza kumbukumbu muhimu za mwenendo wa kesi na hatimae utolewaji wa haki. “Tehama inaimarisha mawasiliano miongoni mwa wadau. Ni rahisi kuwapa taarifa wadau huko waliko wakahudhuria Mahakamani kwa wakati pale wanapohitajika bila taarifa kupotea. Tehama huimarisha maadili ya utoaji wa haki kwa wananchi, vifaa kama CCTV camera na vifaa vingine vya aina hiyo ni muhimu katika kuimarisha maadili ya haki” alisisitiza Masenza.

Katika hotuba ya Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Iringa, mheshimiwa Mary Shangali alisema kuwa wiki ya sheria nchini imelenga Mahakama kujipambanua kwa wananchi na kueleza majukumu ya Mahakama na kutoa elimu kwa wananchi kuwa mahkama kuu ya Tanzania ipo kwa ajili ya wananchi na haki zao.

Mheshimiwa Shangali aliongeza kuwa wiki hiyo inalenga kupima utendaji kazi wa Mahakama. Alisema katika maadhimisho hayo, vituo vya kutolea elimu na kupokelea maoni ya wananchi vimeandaliwa katika shule ya sekondari ya wasichana Iringa, shule ya sekondari ya Miyomboni na chuo kikuu cha Iringa.

=30=    

  

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ‎RC SERUKAMBA AITAKA TRA KUDHIBITI RISITI FEKI, KUHAMASISHA ELIMU YA KODI

    May 19, 2025
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA WA IRINGA.

    May 18, 2025
  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.