Mkuu wa wilaya ya Iringa Komred Kheri James mapema leo amempokea Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mh. George Simbachawene alie wasili wilayani Iringa kwa jukumu la kuhudhuria kikao kazi cha Taasisi ya watunza nyaraka na kumbukumbu TRAMPA.
Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Waziri atafanya jukumu la kufunga kikao kazi hicho kilichofanyika kwa siku tatu kwa lengo la kujengeana uwezo na kukumbushana misingi ya maadili ya taaluma hiyo na majukumu yake.
Akiwasilisha salamu za Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika kikao hicho, Mkuu wa wilay ya Iringa Komred Kheri James amewapongeza viongozi na wanachama wa TRAMPA kwa kufanikiwa kufanya mkutano huo muhimu na amewashukuru kwa kuchagua kufanyia mkutano huo mkoani Iringa, hatua ambayo imesaidia kuchangia uchumi wa wana Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.