• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

TASAF KUNUFAISHA WANAFUNZI WANUFAIKA ILI WASOME KWA BIDII.

Posted on: December 4th, 2017

TASAF KUNUFAISHA WANAFUNZI WANUFAIKA ILI WASOME KWA BIDII

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) una lenga kuhakikisha wanafunzi wanufaika wa mpango huo wanapata huduma za msingi zitakazowawezesha kusoma kwa bidii.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akiongea na wanafunzi wanufaika wa mpango wa TASAF kupitia elimu katika shule ya msingi Kibwabwa iliyopo Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa hivi karibuni.

Ayubu alisema kuwa serikali kupitia TASAF imelenga kumuwezesha mtoto wa kitanzania kufikia malengo yake kupitia fursa ya elimu. Alisema kuwa kutokana na umuhimu wa elimu kwa wananchi, serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dr. John Magufuli iliamua kutoa elimu bila malipo ili watoto wote wa kitanzania wapate fursa hiyo. “Kupitia mpango wa TASAF, serikali inatoa fedha ili wanafunzi wanaotoka katika kaya zisizo na uwezo waweze kugharamia mahitaji ya muhimu kwa mwanafunzi. Mahitaji hayo ni sare, viatu, madaftari, kalamu na masweta ili kujikinga na baridi” alisema Ayubu.

Wakati huohuo, Katibu Tawala Mkoa aliwashukuru kamati ya usimamizi ngazi ya jamii (CMC) kwa kazi nzuri kuwasimamia wanufaika katika kufikia malengo ya mpango wa TASAF. “Tuendelee kusimamia vizuri ili kuleta mafanikio yaliyokusudiwa. Lazima kuwakumbusha wanufaika kuwa pesa za TASAF si za burebure, serikali inaona wananchi wake wanakosa baadhi ya mahitaji ya msingi, hivyo fedha hiyo ni kwa ajili ya kusaidia kufikia mahitaji hayo” alisema Ayubu.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa alifanya ziara maalum ya ufuatiliaji kwa wanafunzi wanufaika wa mpango wa TASAF kupitia elimu katika Manispaa ya Iringa kujifunza changamoto zinazowakabili. Katika ziara hiyo aliambatana na mratibu wa TASAF Mkoa, afisa mipango, mhasibu, mkaguzi wa ndani na afisa habari.

=30=





Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.