• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

WAKUU WA SHULE NA WALIMU WAKUU WATAKIWA KUTHIBITISHA KWA BARUA MICHANGO INAYOENDELEA KATIKA SHULE ZAO

Posted on: January 18th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka wakuu wa shule za sekondari na msingi kuthibitisha kwa barua iwapo kuna michango yeyote inayoendelea katika shule zao kinyume na maelekezo ya serikali.

Agizo hilo amelitoa leo katika kikao cha dharura na wakuu wa shule na walimu wakuu kufuatia agizo la Rais w Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa jana kuhusu michango katika shule nchini.

“Serikali imekwisha elekeza kuwa tunakwenda na elimu bila malipo. Mtu yeyote nayekwenda kinyume na hilo anakwenda kinyume na maelekezo ya serikali. Ni Rais aliyetoa amri hii yeye ndiye mwenye usemi wa mwisho katika mambo yote ya Taifa hili. Yeyote anayekiuka hili atakuwa anafanya kwa dharau” alisema Masenza.

Alisema kuwa waraka wa elimu Namba 3 wa mwaka 2016 kuhusu utekelezaji wa elimu ya msingi bila malipo ulitoa maelekezo ya utekelezaji wa jambo hilo.

Alisema kuwa alikwisha kuwa iwapo kuna hitaji lolote katika shule, libainishwe na jamii na jamii yenyewe ndiyo isimamie utekelezaji wa jambo hilo nje ya utaratibu wa mwalimu mkuu na walimu wengine.

“Nimewaita hapa nijiridhishe, nitamtaka kila mwalimu mkuu wa shule ya msingi na sekondari kwa mkono wake aandike barua kwa mkuu wa Mkoa kuthibitisha kwamba ama upo mchango unaoendelea katika shule yake ama hakuna. Barua zenu zote tutazipitia moja baada ya nyingine. Baada ya hapo tutakuwa na ukaguzi na kuongea na bodi na kamati za shule ili zitumbie kama wanayo michango, michango hiyo iliidhinishwa na nani, ni kiasi gani na kwa madhumuni gani?” alihoji mkuu wa Mkoa.

Aliongeza kuwa eneo lolote litakalobainika kuwa mwalimu mkuu ndiye kichocheo cha huo mchango na yeye ndiye anasimamia hafai na kwa tamko la Rais hana kazi.

Mkuu wa Mkoa aliwataka walimu hao kuacha kuchezea maagizo ya serikali. Aidha, alionesha kuwashangaa waratibu wa elimu ambao katika maeneo yao kuna michango inayoendelea na wao hawafahamu. Aidha, aliwaelekeza waratibu hao kuwepo katika vikao vya bodi na kamati za shule ili kufahamu hli ya mambo inavyokwenda.

=30=

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ‎RC SERUKAMBA AITAKA TRA KUDHIBITI RISITI FEKI, KUHAMASISHA ELIMU YA KODI

    May 19, 2025
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA WA IRINGA.

    May 18, 2025
  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.