• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

WANANCHI WA KATA YA MPANGA TAZARA WAIPA TANO SERIKALI KWA KUWAJENGEA SHULE YA SEKONDARI.

Posted on: December 27th, 2023


Wananchi wa kata ya Mpanga Tazara Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi mkubwa wa ujenzi wa shule ya Sekondari.

Wananchi hao wametoa shukurani zao walipojitokeza katika zoezi la ujenzi wa shule hiyo lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Halima Dendego ambapo wamesema wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi mkubwa katika kata hiyo, mradi ambao unakwenda kutimiza ndoto za watoto wao kwenda shule.

Pia wamesema kuwa uwepo wa shule hiyo, licha ya kupunguza adha ya watoto kutembea umbali wa zaidi ya Km 30, kwenda katika shule ya sekondari Mgololo itasaidia watoto wengi wa eneo hilo kupata Elimu kama ilivyo haki ya mtoto wa kitanzania.

"tumefuhi sana kujengewa shule hapa kijijini, watoto wetu waliteseka kwenda umbali mrefu, hata sisi wazazi hatukuwa na amani pale watoto walipokwenda shuleni mbali hasa kipindi cha mvua, kwa ukaribu huu wa shule, tutakuwa na amani na watoto watafurahi,na pia kutakuwa na mahusiano mazuri kati ya mzazi na mwalimu maana inakuwa shida sana siku mzazi unapohitajika shuleni unakuta gari moshi hiyo siku halipiti hivyo unasubiri mpaka pale gari moshi litakapopita kwa kweli  tunamshukuru Mama Samia " Amesema Gift Kivaya

Akizungumza na wananchi hao Mhe. Dendego amewataka wananchi hao kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani bado itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika kata hiyo.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo Mkuu wa shule ya Sekondari Mdabulo Mwalimu Jumanne Nyaulingo amesema kuwa wamepokea Zaidi ya shilingi milioni mia tano themanii na tatu kwaajili ya ujenzi na kusema kuwa changamoto kubwa waliokumbana nayo ni usafirishaji wa vifaa vya ujenzi na hii imesababishwa na miundombinu ya barabara kutokuwa rafiki kwa usafirishaji wa vifaa hivyo.

Mhe. Dendego amekuwa na ziara ya siku saba ambapo kwa siku tatu amekuweka kambi katika kata ya Mpanga Tazara na Kulala katika Shule ya Msingi ya Mpanga Tazara.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.