• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

BI. HAPPINESS SENEDA, AMEFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA MAENDELEO YA SHULE MBALIMBALI

Posted on: February 17th, 2020

Bi, Happyness Seneda (RAS) amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika shule ya LUGALO sekondari. Na kujione ni jinsi gani shule hizo zimejipanga ili kufaulisha wanafunzi kwa Mwaka huu.


Akisoma taarifa ya ufaulu, Mkuu huyo wa shule amesema ufaulu wastani 92% kwa kidato Cha pili.


Bi Seneda, amewashukuru kwa taarifa hiyo na kusimammia ujenzi huo, na amewataka Halmashauri ya Manispaa kutenga bajeti ili kurabati nyumba za Waalimu.


Pia amewataka kuongeza spidi hasa katika kuongeza ufaulu maana LUGALO ni shule kongwe hivyo hafurahishwi na matokeo hayo. Amekili Mwalimu Mkuu kuwa ni kweli ufaulu uko chini sana, lakini kuanzia sasa wamejipanga kwa kuanza na wanafunzi kukaa kambi na kufundisha wanafunzi. Pia na kudhibiti Waalimu ambao nao ni watoro.


Akifafanua Afisa Elimu wa Wilaya ya Manispaa Bi Tupe Kayinga Asema changamoto kubwa wanayopata sababu kwa manispaa hawana hostel kabisa hivyo kufanya  utoro kuwa mkubwa zaidi. Lakini wamekubaliana mwezi 6 watakuwa na makambi kwa pamoja kwa muda wote wa likizo na wakifungua tu watafanya mthiani wa mock. Na Kuna fomu wamezianzisha maalumu kwa ajili ya kudhibiti Waalimu ili kujua Kama anafundisha vipindi vyake kwa wakati, lakini pia wamegundua tatizo la utoro linasababishwa na ukosefu wa chakula, na kila mzazi  ataleta chakula badala ya mchango wa fedha.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, amesema lengo la Mkoa ni kushika nafasi ya kwanza. Amesema kumekuwa na changamoto kubwa sana  hasa shule za mjini sababu Waalimu wako bize na mambo yao.


Bi Seneda (RAS) ameongea na Waalimu wa sekondari ya LUGALO na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya hasa katika ufaulu ndani ya Mkoa wa Iringa. Lengo la ziara yake nikuendelea kuona mikakati waliyoiweka inatekelezwa  ili kuongeza ufaulu. Hata hivyo amewaambia Waalimu hao kuwa bado hajaridhishwa na ufaulu katika shule hiyo ambao unapelekea kushusha Mkoa katika ufaulu huo.


Kuna changamoto sana kwa Waalimu zaidi katika  utoro, upungufu wa Waalimu wa sayansi siyo sababu kubwa ni kujituma zaidi kwa Waalimu hao ili wanafunzi wafaulu vizuri. Akitoa mfano huo na kuwatia moyo Waalimu amesema hata yeye alishawahi kuwa mwalimu wa chemistry na biology lakini leo ni katibu Tawala wa Mkoa, hivyo wasikate tamaa sababu hawajui kesho yao.


Akisema mwalimu Mlilla Chigomelo amsema tatizo kubwa kupandishwa madaraja na nauli za likizo ni tatizo kubwa hii inavunja morali ya kazi.


Naye mwalimu Kasumuni, amesema kumekuwa na tatizo kubwa hasa muongozo wa kuwataka wanafunzi wenye ulemavu wa macho kusoma sayansi, wakati hawaoni future yao ya baadae, sababu masomo ni mengi sana, Na shida nyingine uhaba wa vifaa kwa watoto wenye ulemavu wa macho ambapo mpaka Sasa Wana mashine 28 tu nazo ni mbovu.


Pia amezungumzia ushirikiano kati ya Waalimu na Wazazi, maana Wazazi wamewaachia jukumu hilo la watoto Waalimu peke yao, mfano mtoto/wanafunzi  wakirudi nyumbani wanaangalia tv tu na inapelekea kulala usiku sana na wanapokuwa darasani wanasinzia tu.


Pia Kuna upungufu mkubwa wa vitabu vya chemistry hivyo inawawia vigumu kuwashawishi wanafunzi kusoma sayansi.


Akifafanua juu ya changamoto hizo za Waalimu Afisa Elimu wa manispaa amesema mpaka sasa wamekwisha wapandisha madaraja na mishahara yao inarekebishwa. Kuhusu malipo ya fedha za likizo itatolewa kwa awamu  kulingana na fedha wanazopata.


Akiwa shule ya sekondari ya wasichana (Iringa Girls) Bi. Seneda, amesomewa Taarifa ya maendeleo ya mradi na ufaulu wa shule hiyo.


Amepongeza sana kwa Mkuu wa shule hiyo bi Nkondola kwa kuendelea  kupunguza deni la shule alilolikuta milioni 400, ambapo amekwishalipa milioni 200.


Bi Seneda, amewataka Halmashauri ya Manispaa kujenga uzio wa shule hiyo ni muhimu sana. Ambapo Katibu Tawala Mkoa naye ameahidi kuwaletea saruji( cement) mwezi wa 3.


Pia Bi. Seneda, ametembelea shule ya sekondari Tosamaganga.


Akisoma taarifa ya shule Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mgimwa, amesema shule inapanda kwa ufaulu na wanamkakati wa kufuta daraja la nne na 0.


Amsema ndugu Mgimwa kuwa ukarabati unaendelea ambapo mpaka sasa majengo 13 yapo kwenye hatua nzuri. Fedha iliyotumika milioni 53.


Bi. Seneda amewapongeza kwa usimamizi wa ukarabati wa majengo hayo.


Pia bi Seneda, alitakujua changamoto zao zinazopelekea kushuka kwa ufaulu, ndi Mwalimu Mkuu Mgimwa, alisema tatizo kubwa ni ukosefu wa maji kwa ajili matumizi ya wanafunzi na ukosefu wa vifaa vya sayansi kwa ajili ya mafunzo ya wanafunzi.


Hivyo bi Seneda, amemtaka mwalimu Mkuu huyo ndugu Mgimwa, kuongeza kasi sana katika ufaulu. Amemuagiza Afisa Elimu wa Wilaya ya Iringa kufatilia kwa kina juu ya shule hii, maana hakuna Mpango kazi wa ufaulu.


Bi Seneda, amewataka kuona mikakati mipya kwa ajili ya kuongeza ufaulu maana shule hii ni kongwe sana na ina historia nzuri toka zamani sasa hataki kuona historia inaharibika. Pia amewaagiza akae na Waalimu na wajue nini changamoto zao na ipi mikakati yao kwa ajili ya kuongeza ufaulu shuleni hapo.


Amewataka kutengeneza timu kazi kuanzia ngazi ya Wilaya hadi shuleni itakayoleta morali na hatimaye itasaidia kuleta ufaulu.


Imetolewa na:

Ofisi ya Habari Mkoa,

Humphrey Kisika.



Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.