Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James amesema Serikali kwa kushirikiana na makampuni ya mawasiliano inaendelea kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi wote Mkoa wa Iringa kwani maendeleo yoyote yale yanakuja kupitia huduma nzuri ya mawasiliano.Akizungumza Julai, 01,2025 mara baada ya kutembelewa Ofisini kwake na Kampuni ya Vodacom ambayo mwaka huu inaadhimisha miaka 25 ya utoaji wa huduma nchini Tanzania,ambapo Mhe. Kheri amesema kuwa kwa maendeleo yanayoendelea kufanyika nchini kwa sasa makampuni haya ya Mawasiliano yanahitaji kuendelea kukuza huduma za mawasiliano kwa kusogea baadhi ya sehemu ambazo bado zina changamoto ya mawasiliano."Huduma zikiwa Bora zinaturahisishia kuwahudumia Wananchi kwasababu bila mawasiliano hatuwafikii wala wao hawatufikii hivyo tunavyokuwa na huduma za uhakika tunakuwa na uhakika wa kuwafikia watu na kuwahudumia watu na kutatua changamoto kwa wakati"Pia ameitaka kampuni hiyo kuendelea kujitokeza kwenye jamii kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali huku wakiendelea kuboresha miundombinu ya mawasiliano.
Zaidi ya washiriki 10,000 wanatarajiwa kushiriki mashindano ya kitaifa ya michezo kwa shule za msingi na sekondari, UMITASHUMTA na UMISSETA, yatakayofanyika mkoani Iringa kwa mara ya kwanza mwaka 2025, tukio linalotajwa kuwa la kihistoria kwa Mkoa wa Iringa .Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba, amethibitisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa mashindano hayo ni fursa adhimu kwa mkoa wa Iringa, huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiamini Iringa kuwa mwenyeji wa tukio hilo la kitaifa.“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutupatia heshima hii kubwa, Kwa mara ya kwanza Iringa itakuwa mwenyeji wa mashindano haya makubwa, baada ya kuwa yamefanyika mkoani Tabora kwa mfululizo Kwa miaka mitatu ,” amesema Mhe. Serukamba.Kwa mujibu wa ratiba rasmi, mashindano ya UMITASHUMTA yataanza tarehe 08 Juni hadi 17 Juni 2025, yakifuatiwa na mashindano ya UMISSETA yatakayodumu kuanzia tarehe 08 hadi 30 Juni 2025.Mashindano hayo yanatarajiwa kukutanisha wanafunzi, walimu wa michezo, maafisa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka sekta ya elimu na michezo kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Michezo itakayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, netiboli, pamoja na mchezo wa kengele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Aidha, burudani ya muziki wa kizazi kipya pia itakuwepo, ikitumbuiza na kuhamasisha washiriki na mashabiki.Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ni pamoja na Shule ya Sekondari Wasichana Iringa, Shule ya Sekondari Lugalo, pamoja na Chuo cha Ualimu Klerru.Aidha Mhe. Serukamba amewataka wananchi wa Iringa kutumia vyema fursa hii kwa kutoa huduma mbalimbali zitakazowawezesha kunufaika kiuchumi.“Wananchi wanayo nafasi ya kipekee ya kunufaika na wageni watakaofika hapa. Huduma za malazi, vyakula, usafiri na biashara ndogondogo zote zitahitajika. Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia ufunguzi rasmi wa mashindano hayo utakaofanyika tarehe 09 Juni 2025
Ikiwa ni mwendelezo wa ziara za Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Januari 27, 2025 ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kufanya Mkutano wa hadhara Kijiji cha Itunundu, tarafa ya Pawaga huku akiwahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidiiAkizungumza wakati wa mkutano huo na wanakijiji Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa changamoto zote zilizowasilishwa na wanakijiji zitafanyiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo huku akiwataka wanakijiji wa Itunundu kufanya kazi kwa Bidii kupitia miradi ya maendeleo iliyopo kijijini hapo."Niwaombe mfanye kazi kwa bidii Serikali inawekeza kwenye umwagiliaji, Serikali inawekeza kwenye mashule inawekeza kwenye umeme, inawekeza kwa kila kitu lakini kama wewe mmoja mmoja hufanyi juhudi bado tutaendelea kuilaumu Serikali wakati Serikali imefanya kila kitu."Sambamba na hayo Mhe. Serukamba ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa namna walivyopambana katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.