• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

IRINGA YAJIVUNIA HIFADHI YA RUAHA

Posted on: February 11th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Iringa

Mkoa wa Iringa unajivunia hifadhi kubwa ya taifa ya Ruaha yenye upekee unaovutia watalii wa ndani na nje ya nchi kuitembelea.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akisoma taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Iringa kwa Makamu wa Rais, mama Samia Suluhu Hassan jana katika rest house ya NSSF mjini Iringa.

Masenza alisema kuwa Mkoa wa Iringa una hifadhi za taifa mbili hifadhi ya Taifa Ruaha na hifadhi ya Taifa ya Udzungwa. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ina ukubwa wa Kilometa za mraba 20,226. “Asilimia 38 ya eneo la hifadhi ya Ruaha ambayo ni sawa na Kilometa za Mraba 777 zipo katika Mkoa wa Iringa. Hifadhi ya Ruaha ni kubwa kuliko hifadhi zote za Tanzania na ya pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ile ya Kafue iliyopo nchini Zambia” alisema Masenza. Aliongeza kuwa upekee wa hifadhi hiyo ni uwepo wa mwingiliano wa bioanuwai za kusini na kaskazini mwa Tanzania.

Akiongelea hifadhi ya Taifa ya milima ya Udzungwa yenye ukubwa wa Kilometa za mraba 1,990 ambapo asilimia 80 sawa na Kilometa za mraba 1,596.8 za eneo lote la hifadhi ya Milima Udzungwa ipo katika Mkoa wa Iring alisema kuwa hifadhi hiyo ni hifadhi pekee iliyopo katika milima ya tao la mashariki. “Hifadhi hii ina hazina ya aina nyingi za mimea, ndege, vyura wa Kihansi na wanyamapori ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote duniani. Baadhi ya viumbe hao ni mbega mwekundu wa Iringa (Iringa red colobus monkey) na Sanje Crested mangabey” alisema Masenza.

=30=

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.