• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

IRINGA YAPONGEZWA USIMAMIZI UJENZI WA HOSPITALI WILYA KILOLO

Posted on: January 29th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa imepongezwa kwa usimamizi makini unaozingatia thamani ya fedha katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo unaoendelea.

Pongezi hizo zilitolewa na makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa, Mwanne Mchemba alipokuwa akiongea na wataalam wa Mkoa wa Iringa na Wilaya ya Kilolo katika kumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo baada ya kamati yake kukagua ujenzi wa hospitali hiyo hivi karibuni.

Mchemba alisema kuwa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa imefanya kazi nzuri kusimamia ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo. “Najua mipango mizuri ya ujenzi wa hospitali hii mliiratibu vizuri tangu mwanzo ndiyo sababu ujenzi unaenda vizuri. Kamati yangu imeridhishwa na hatua ya ujenzi kwa kuzingatia thamani ya fedha” alisema Mchemba. Alipongeza wazo hilo kuwa linalenga kuboresha afya za wananchi wa Wilaya ya Kilolo na taifa kwa ujumla kwa kuwapatia huduma bora za afya.

Mchemba aliishauri ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa kipaumbele katika ujenzi wa chumba cha upasuaji na chumba cha kuhifadhia maiti. Alisema kuwa ujenzi wa majengo hayo utasaidia kuiwezesha hospitali hiyo kuanza ikiwa na maeneo muhimu ya utoaji huduma. Aidha, alielekeza hospitali hiyo kupatiwa gari la wagonjwa. “Kutokana na jiografia ya Wilaya ya Kilolo ni muhimu hospitali ya Wilaya kupewa gari la wagonjwa. Gari hilo ni muhumu sana kwa sababu litasaidia kuokoa maisha ya wananchi watakaohitaji huduma ya haraka na dharura hospitali hapo” alisema Mchemba.  

Awali katika taarifa ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo iliyosomwa na mganga mkuu wa Wilaya, Dr. Mohamed Mang’una alisema kuwa mradi huo ulianza kwa gharama ya shilingi 259,451,899 kugharamia ujenzi awamu ya kwanza na ya pili. Alisema kuwa kupitia ruzuku ya maendeleo ya serikali za mitaa kwa mwaka 2011/2012 zilitolewa shilingi 145,744,500 na mwaka 2012/2013 zilitolewa shilingi 113,707,399 kujenga jengo la wagonjwa wa nje.

Hospitali ya Wilaya ya Kilolo imelenga kuhudumia wakazi wanaokadiriwa kuwa 229,146 kutokana na sense ya watu na makazi ya mwaka 2012.

=30=

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.