• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

IRINGA YATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKA

Posted on: May 15th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Mkoa wa Iringa unatekeleza agizo la serikali ya awamu ya tano la kuufanya ushirika kuwa nguzo ya kuwasaidia wakulima.

Kauli hiyo ilitolewa na kaimu Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Iringa, Robert George alipokuwa akisoma taarifa ya hali ya ushirika katika mkoa wa Iringa katika jukwaa la ushirika mkoa wa Iringa lililofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa hivi karibuni.

George alisema kuwa mkoa unaendelea kutekeleza agizo la serikali la kujenga ushirika imara unaomsaidia mkulima. “Katika kuhakikisha kuwa ushirika unakuwa imara na kuongeza idadi ya wanachama kama lilivyo agizo la Serikali ya awamu ya tano ambalo linatuhitaji sisi kama wasimamizi wa ushirika kuhakikisha kuwa ushirika unakuwa ndio nguzo ya kumsaidia mkulima. Kwa mwaka 2017/2018 jumla ya vyama vya ushirika 8 vimeandikishwa zikiwepo SACCOS 5 na AMCOS 3” alisema George.

Uhamasishaji wa vyama vilivyosinzia ili viweze kuamka umefanyika kupitia chama kikuu cha ushirika na maafisa ushirika, jumla ya vyama vya ushirika vitano vimeamka ambavyo ni Magulilwa AMCOS Ltd, Ipilimo AMCOS Ltd, Matanana AMCOS Ltd, MVIKIMA SACCOS Ltd na Ikimo AMCOS Ltd.

Akiongelea utekelezaji wa maagizo ya serikali kuhusu mazao ya kimkakati, Mrajis msaidizi mkoa wa Iringa alisema kuwa halmashauri zimehamasisha kilimo cha mazao ya korosho na pamba katika kata za Nzihi na Malengamakali kupitia vyama vya ushirika vya Nzihi mixed na Usolanga.

Aliongeza kuwa mkoa unaendelea kusimamia na kuviimarisha vyama vya ushirika vitatu vinavyojishughulisha na kilimo cha chai. Vyama hivyo alivitaja kuwa ni Mkonge Amcos, Sawala Amcos na Luhunga Amcos. “Kwa mwaka 2017/2018 jumla ya vijiji vitano vimehamasishwa kuanzisha vyama vya ushirika vya kilimo cha chai katika halmashauri ya Mufindi. Vijiji hivyo ni Igoda, Kibao, Udumka, Mninga na Makalala” alisema George.

Halmashauri zinaendelea kuhamasisha kilimo cha kahawa, korosho na pamba aliongeza. “Kwa msimu huu wa mwaka 2017/2018 wakulima wa halmashauri wilaya ya Iringa wamepanda karosho kwa wingi hivyo, kwa maeneo yote yaliooteshwa korosho uhamasishaji wa kuanzisha vyama vya ushirika utafanyika katika msimu wa 2018/2019. Kutokana na jiografia ya maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wetu mazao yote ya kimkakati yanaweza yakastawishwa na wanachama wa vyama vya ushirika” alisema George.

Jukwaa la ushirika ni jukwaa la pili kufanyika ngazi ya mkoa, likishirikisha Katibu Tawala Mkoa, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa, wadau wa taasisi za kifedha na wanaushirika.

=30=

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.