• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

KAMATI ZA UENDESHAJI MITIHANI MKOANI IRINGA ZAPONGEZWA KUDHIBITI UDANGANYIFU

Posted on: December 26th, 2017

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Kamati za uendeshaji wa mitihani ngazi za Wilaya na Mkoa zimepongezwa kwa usimamizi madhubuti wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na kudhibiti udanganyifu.

Pongezi hizo zilitolewa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akifungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa jana.

Ayubu alisema kuwa mwaka 2017 Mkoa wa Iringa haukukumbwa na tuhuma za udanganyifu. “Kipekee nazipongeza kwa dhati kamati za uendeshaji wa mitihani za Wilaya na ya Mkoa kwa usimamizi mzuri. Nitoe wito kuwa usimamizi huu uendelee  kwa mitihani ya kitaifa ya ngazi zote ili kuepukana na suala la udanganyifu ambalo kwa kiasi kikubwa madhara yake ni makubwa kwa mwanafunzi mwenyewe, mwalimu aliyehusika na udanganyifu na Taifa kwa ujumla” alisema Ayubu.

Akiongelea idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani, alisema kuwa

watahiniwa 24,784 (wavulana 11,421 na wasichana 13,363) sawa na 99.5% walifanya mtihani. Aliongeza watahiniwa 20,606 (wavulana 9513 na wasichana 11,093) sawa na asilimia 83.14 wamefaulu mtihani huo. Alisema wanafunzi walioshindwa kufaulu mtihani huo ni 4,178 ikiwa wavulana 1,908 na wasichana 2,270 sawa na asilimia 16.86

“Kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 0.27 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana ambapo ufaulu ulikuwa ni 82.87%. Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wadau wote wa elimu katika Mkoa wetu ambao mchango wao ni mkubwa kwa ongezeko hili la ufaulu na kuufanya Mkoa wetu kuwa wa Nne (4) kitaifa kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara alisema Ayubu.

Mwaka 2017 Mkoa wa Iringa ulikuwa na watahiniwa 24,905 waliosajiliwa kufanya mtihani, wakiwemo wavulana 11,490 na wasichana 13,415 katika shule 481.

=30=



Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.