• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru arizishwa na ubora wa Miradi ya Halmashauri ya Mufindi

Posted on: May 24th, 2018

Na. Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji -Mufindi

Jumla ya Miradi 06 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.199 imezinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi pamoja na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru, ulipokimbizwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi, huku wakimbiza Mwenge kitaifa wakiridhishwa  na viwango vya miradi husika na kutanabaisha kuwa vinaendana na thamani ya fedha zilizotumika.

 Ukiwa katika Halmashauri  ya Wilaya ya Mufindi  Mwenge wa Uhuru  umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa   Sekondari  ya Igombavanu, umezindua klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Igombavanu,  ujenzi wa zahanati ya Kijiji pamoja na kukagua mradi wa hifadhi ya mazingira katika msitu wa kupandwa wa Halmashauri  Kijiji cha Mtili,  umezindua ujenzi wa Barabara ya lami Kitiru- Itulituli yenye urefu wa Kilomita 14.972, na mradi wa kilimo na mifugo wa mwananchi  kata ya Igowole.

Akizungumza wakati wa kutoa ujumbe wa Mwenge,kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu. Charles Francis Kabeho, amewahamasisha wananchi kuwekeza katika elimu kwa  kugharamia mahitaji muhimu ya Watoto wao, kama mavazi, viatu, Madaftari  sanjari na kuchangia mchango wa Chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa  chini ya ujumbe mkuu wa mbio za Mwenge 2018 “ELimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu”

Aidha, ameendelea Kuhamasisha kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, VVU/UKIMWI, dawa za kulevya na mapambano dhidi ya Malaria.

“Maambukizi ya UKIMWI yameendelea kuwa tatizo kubwa katika Mkoa wa Iringa, mkiongozwa na Mkoa wa Njombe wenye asilimia 11.4, wakati ninyi mnashika nafasi ya pili kitaifa kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 11.3 hivyo, inatupasa tuchukue hatua za kubadili tabia kwani hali hii ikiendelea hivi ni hatari kwa maendeleo ya Taifa’’ alisema Kabeho

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, Kupitia risala ya utii  kwa mkuu wa nchi, amemhakikishia  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwamba, Wilaya yake, itaendelea kutekeleza  Maagizo mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda, usimamizi wa Mbolea ya ruzuku, kuokoa mifumo ya kiikolojia ya bonde la Mto Ruaha mkuu pamoja  na suala la Waalimu Kutojihusisha na michango ya Wazazi Shuleni .

Mkesha wa Mwenge wa Uhuru uliambatana na zoezi la upimaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI na katika upimaji huo,  jumla ya watu 435 walijitokeza kujua Afya zao, kati yao wanaume ni 232 na Wanawake ni 203 ambapo katika zoezi hilo ni watu 04 tu ndio waligundulika kuwa na maabukizi ikiwa ni Wanawake 02 na Wanaume 02.


=30=

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.