• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Makamu wa Rais Kuanza Ziara ya Siku Tano Mkoani Iringa

Posted on: February 8th, 2018

Anaandika Atley Kuni- TAMISEMI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanza ziara ya Kikazi kwa muda wa Siku tano Mkoani Iringa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenda kwa vyombo vya  habari na Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza, imesema ziara hiyo pamoja na mambo mengine vilevile, Makamu wa Rais atapata fursa yakuongea na kusalimiana na wananchi wa mkoa huo

Masenza amesema, Mapokezi ya Mheshimiwa Makamu wa Rais yatafanyika kwenye Kijiji cha Kising’a Wilaya ya Iringa majira ya saa 3.45 asubuhi.

Ndugu zangu mara baada ya mapokezi  Makamu wa Rais atafungua wodi ya Kissing’a lakini pia atakagua upanuzi wa kiwanda cha IVORY, sambamba na kukagua kiwanda cha ufungashaji mazao ya Mbogamboga na Jioni ya siku hiyo hiyo atapokea  taarifa ya Mkoa na kuzungumza na viongozi wa taasisi mbali mbali mkoani humo.

Mheshimiwa Masenza amefafanua kuwa katika siku yake ya pili Mheshimiwa  Makamu wa Rais ataelekea Wilaya ya kilolo ambapo atazindua jengo la utawala shule ya Sekondari kilolo na atafanya mkutano wa Hadhara katika eneo la Ilula.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkuu wa Mkoa na kusambazwa katika vyombo vya habari imeonesha siku tarehe 11Februari 2018 Mhe. Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi katika maabara kwenye shule ya Sekondari Mgololo na atafungua zahanati ya Kijiji cha Mtili na kukagua kiwanda cha utengenezaji Mkaa Mafinga.

Masenza alifafanua kwamba katika siku zote hizo  Mheshimiwa Makamu wa Rais atapata pia fursa ya kuzindua mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini (REGROW) ambapo Mkoa wa Iringa ni kitovu cha Utalii utakaofanyika kwenye  eneo la kihesa kilolo kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi na majira ya saa  8:00 Mchana atafanya Mkutano wa Hadhara Mwembetogwa katika Manispaa ya Iringa.

Hata hivyo Mh. Masenza amefafanua kuwa, siku ya tarehe 13 Januari, 2018 atafanya majumuisho kabla yakuondoka mkoani humo.

Mh. Masenza amewaomba wananchi wa Iringa kujitokeza kwa wingi ili kumlaki kiongozi huyo wa Kitaifa.

“Natoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa shamrashamra, nderemo na vifijo na furaha tele wakati wa mapokezi na maeneo yote ya miradi anayotembelea ambapo atapata fursa ya kuwasalimia wananchi” amenukuliwa Masenza.

=30=


Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.