• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Iringa Ally Hapi akutana na Wadau wa Elimu katika kujadili maendeleo ya elimu Mkoani humo.

Posted on: December 11th, 2019

Akifungua kikao hicho Mheshimiwa Hapi amesema, vikao kama hivi vya kukutana na Wadau wa Elimu ni muhimu sana. Hapa tutajua changamoto na mafanikio mbalimbali yaliyopo katika Sekta ya Elimu.

Malengo ya kufanya kikao ni kutathimini hali ya maendeleo ya elimu, kuainisha mafanikio na changamoto za Sekta ya Elimu, mbinu na mikakati ya kutatua changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu, amesema Mheshimiwa Hapi.

Pia kupima fursa za Watendaji wote wa Sekta ya Elimu, kufanya mipango Mkoa huu uwe juu kielimu. Jukumu la msingi ni kuangalia watoto na changamoto zao.

Ameongeza kusema kuwa, hiki kikao ni muhimu sana kwetu na inatakiwa kikae mara mbili kwa mwaka na siyo mara moja kama ilivyozoeleka.

Mheshimiwa Hapi amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Mufindi na Watendaji wake katika Halmashauri za Mufindi na Mafinga Mji kwa kusimamia vema ujenzi wa madarasa na kufanya wanafunzi wote walichaguliwa kuingia Kidato cha Kwanza, kuanza shule kwa wakati. Kisha amewasisitiza Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Iringa Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuharakisha vyumba vya madarasa ili watoto waliofaulu kuanza kidato cha kwanza, kwani katika Halmashauri hizo ina jumla ya wanafunzi 3,480 wamekosa kupangiwa kuanza kidato cha kwanza kwa ajili ya upungufu wa madarasa.

Mheshimiwa Hapi amesema, hakutakuwa na likizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara ya Elimu na Wakuu wa Shule ambao katika maeneo yao bado kuna changamoto za upungufu wa vyumba vya madarasa, ili wafanye kazi usiku na mchana kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo.

Amemaliza kwa kusema kuwa, kila shule ya msingi na sekondari kuwepo na mlezi wa wanafunzi ambaye atakuwa rafiki, mwenye busara, na kuweza kusikiliza matatizo ya watoto. Kwani watoto wengi wanakabilliwa na wimbi la matatizo ya ubakaji, kulawitiwa na unyanyasaji wa kijinsia na kingono lakini hawana mahali pa kusema matatizo wanayokabiliana nayo. Ameagiza ndani ya mwezi mmoja kila Mkuu wa Shule awe ameleta mapendekezo ya mlezi  kwa Afisa Elimu Mkoa. Dawati la Jinsia na Ustawi wa Jamii washirikiane kutoa semina kwa walezi hawa ili wawe na uelewa wa jinsi ya kukabiliana na matatizo ya wanafunzi.

Imetolewa na Ofisi ya Habari Mkoa,

Humphrey Kisika.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.