• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi Aongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani Kujadili Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Mji wa Mafinga Tarehe 22 Mei, 2020.

Posted on: May 22nd, 2020

Mheshimiwa Hapi ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kupata hati safi tangu ilipoanzishwa,  kwani ni maelekezo ya Serikali kuwa katika Halmashauri zote lazima zijibu hoja za Mkaguzi wa Serikali.

Mheshimiwa Hapi ameendelea kusema kuwa, Mji wa Mafinga nimekuja mara nyingi, hivyo naujua vizuri na Madiwani hawa nimefanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa sana. Kwa kweli mnafanya vizuri kila jambo, kama elimu, mapato, miradi mbalimbali kama vituo vya afya na kupelekea kupata hati safi.

Hapi amesema katika ziara yangu ya #IringaMpya nimeona kero ni chache sana, ni kero 27 tu ndizo zilizokuwepo, hii inaonesha kuwa mnafanya kazi vizuri. Mshikamano na kujituma ndiyo mafanikio yenu. Katika hoja 33 zimebaki hoja 5 tu, naomba wataalamu wazishughulikie ili hoja hizi zifutwe.

Mheshimiwa Hapi amewakumbusha kuwa, Vifaa vilivyoletwa vya kiasi cha Tsh. 15 milioni kwa ajili ya Kituo cha Afya Ihongole, vianze kufanya kazi ili wananchi waweze kupata huduma bora. Jambo la madeni ya watmishi na wakandarasi siyo mbaya sana, ninaomba yalipwe hasa kwa watumishi ili wapate morali ya kufanya kazi. Pia sekta ya elimu imekuwa na changamoto kutokana na idadi ya uandikishaji, hivyo agenda yenu kuu katika vikao iwe ni elimu, kuongeza madarasa, kuweka benki ya matofali ili kusiwepo na upungufu. Katika Mkoa wetu kimapato tuko vizuri sana kwa Halmashauri zote.

Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli imeendelea kutoa miongozo mbalimbali ili kutekeleza majukumu. Halmashauri hii imejigawa ili kurahisha utoaji wa huduma kwa wananchi. Tuendelee kushirikiana kutatua shida za wananchi ili kusiwepo na vita kati ya Mafinga Mji na Halmashauri ya Wilaya Mufindi.

Nawaomba Madiwani kuhamasisha wananchi kuchangia katika mfuko wa CHF iliyoboreshwa kwani ni mkombozi kwa wananchi, hivyo watu wajiunge kwa wingi katika mfuko huu.

Nawaomba mambo makubwa mawili:-

  • Serikali ya Mheshimiwa JPM imefanya mambo makubwa sana, ikiwemo jengo hili la Halmashauri, miradi mikubwa ya maji, hospitali n.k. Hivyo twende tukayasemee kwa wananchi ili wajue tunapoenda kwenye uchaguzi iwe kazi nyepesi, na wajue mafanikio haya.
  • Covid-19 – Mji huu upo barabarani, hivyo kuna muingiliano mkubwa wa watu kibiashara. Naomba watu waendelee kuchukua tahadhari. Rais wetu ana mapenzi makubwa na nchi, angefuata taratibu za nchi nyingine za kufunga uchumi, basi uchumi ungekuwa vibaya sana.
  • Sekata isiyo rasmi ambayo ni kundi kubwa la wangekuwa wameathirika sana. Kuba baadhi ya makampuni wamepunguza wafanyakazi. Ninawahakikishia kuwa, Rais wetu yupo vizuri aliona mbali sana, msimamo wake umetusaidia sana kuwa salama. Japo corona itaendelea kuwepo hivyoi tunaishi nayo kwa kuchukua tahadhari. Uongozi ni mgumu sana na unahitaji busara, Rais wetu ana msimamo na ana mapenzi kwa nchi.

Mwisho Mheshimiwa Hapi amewatakia kila la heri katika uchaguzi mkuu ujao.

Pia Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda naye alikuwa na haya ya kusema, kwanza kwa kuwapongeza Mafinga Mji kwa kuhamia katika jengo lao jipya, pili aliwapongeza kwa kupata kupata hati safi, tatu amewapongeza kwa ukusanyaji mzuri wa mapato na kuw Halmashauri kushika nafasi ya 19 kati ya Halmashauri 185 nchini. Nne amewapongeza kwa kujibu vizuri hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, tano amewapongeza kwa kutokuwa na madeni kwa Madiwani.

Pamoja na pongezi hizi, Mheshimiwa Katibu Tawala amewaomba kuendelea kushughulikia hoja za kamati, na kutosubiri hadi waitwe na kamati ya LAAC. Amesema kwa kutumia Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (Council Management Team – CMT) kuhakikisha hoja zote zinajibiwa kikamilifu. Pia amesisitiza kushughulikia hoja za Mkaguzi wa Ndani, kwni kufanya hivi inapunguza hoja za LAAC.

Mwisho ameomba tuendelee kupambana na janga la corona, huku tukichukua tahadhari na kuondoa hofu. Pia kuhakikisha tunafanya kazi ili uchumi wetu usishuke, hasa katika fursa za kilimo, na kuwatakia heri katika uchaguzi ujao.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.