• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi Aongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani Kujadili Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Wilaya Mufindi Tarehe 28 Mei, 2020

Posted on: May 28th, 2020

Mheshimiwa Hapi pamoja na salamu mbalimbali alianza kwa Mwenyezimungu kwa rehema alizotujali, na kuwepo katika Baraza la Mwisho la Madiwani kwa kujadili hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Mheshimiwa Hapi amesema, Serikali imetoa maelekezo ya matumizi ya fedha za ziweze kukaguliwa, pia ilitoa kwa Kamati ya Bunge kukagua mahesabu na miradi mbalimbali. Mheshimiwa Hapi amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kusimamia vema kwa kadiri ya taratibu zinavyotakiwa, pia Baraza la Madiwani, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na watendaji wote wa Halmashauri kwa kupata hati safi. Ushirikiano wao ndiyo umewafikisha hapa tulipo na kuwaasa kutojibweteka kwa vile wamepata hati safi.

Katika hoja 36 na 11 za miaka ya nyuma na kuleta jumla ya hoja 47, na hoja

28 zimefutwa na kubakia hoja 19, pia maagizo ya LAAC kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo kabla ya mwaka wa fedha kwisha.

Kw upande wa madeni; Halmashauri ina utaratibu wa kukusanya mapato kwa mashine na kupeleka benki, kiasi cha Tsh. 232 milioni hazijaenda benki kama taratibu zinavyosema. Wale ambao walikusanya pesa hawajapeleka benki ili ziwe kwenye mfumo wafanye haraka iwezekanavyo kupeleka benki. Kuna watu waliofanya ubadhilifu wachukuliwe hatua haraka sana bila kuwaonea haya. Maana kuna utaratibu kuwa, mtu akifanya ubadhilifu mnamuambia urudishe au mnakata kwenye mshahara wake hadi deni litakapokwisha, hii tabia sitaki kuisikia tena, wachukuliwe hatua kali za kisheria. Halmashauri ina madeni ya watumishi na wakandarasi, kiasi cha Tsh. 395.1 milioni. Lipeni madeni haya hasa watumishi ili wapate moyo wa kufanya kazi kwa bidii.

Tulipokea vifaa kutoka MSD kwa ajili ya hospitali ya Malangali, baadhi ya vifaa havijaanza  kutumika, nahitaji vianze kutumika kwa kuwapa wananchi huduma bora. Pia usimamizi wa mali za Halmashauri, kuna magari hayatumiki au ni chakavu, kama yanatengenezeka basi yatengenezwe na kam haiwezekani yaondolewe kwenye mfumo na yasisomeke.

Nawapongeza kwa kutoa 10% kwa ajili ya mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu, nawapngeza sana kwa kujali vikundi. Endeleeni kusimamia matumizi ya fedha hasa kwenye akaunti ya Amana.

Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo makubwa sana kuleta miradi mikubwa kama maji, hospitali, barabara, elimu n.k. Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wan chi, hakikisheni miradi yote inakamilika ili kusiwepo na maswali kwa wananchi hasa upande wa elimu kwani uandikishaji ni mkubwa sana.

Pia nawapongeza kwa kukusanya mapato kwa kufikia 88% hadi kufikia leo. Sote tunajua bila mapato hana huduma. Mkurugenzi na timu yako endeleeni kusimamia, kabla ya kufika mwisho wa mwaka iwe imefika 100%. Mkurugenzi kaza uzi katika suala hili, asitokee mtu anakwepa kulipa ushuru, kodi ni lazima vilipwe. Nasisitiza kufuata taratibu za fedha na manunuzi, hii itasaidia kudhibiti hoja. Pia nawapongeza kwa kulipa madeni ya madiwani.

Maagizo:

  • Suala la ushirikiano, watumishi, viongozi, Madiwani na watendaji, msiwe tayari kugawanyika, kuna Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Mwenyekiti kwani sote lengo letu ni moja. Katika kufanya hivyo tutafanya mambo makubwa na mazuri. Pia kushirikiana na Halmashari ya Mji w Mafinga kwani katika kutoa huduama lazima tuingiliane.
  • CHF iliyoboreshwa kwa wananchi waendelee kujiunga ili wapate matibabu bora hospitalini.
  • Nawapongeza Halmashauri zote kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, Mufindi imekusanya 88%, Kilolo 101%, Mafinga Mji 96%, Manispaa 105% na Iringa DC 89% hadi kufikia leo. Najivunia kuongeza Mkoa ambao upo vizuri katika uchapaji kazi.
  • Katika ziara yangu ya #iringampya naona kero zimepungua sana, tofauti na ile awamu ya kwanza, nawapongeza kwa kuchapa kazi na kutatua kero za wananchi.
  • Tarehe 12/3/20 nilipokea ripoti ya mgogoro wa chai kati ya Halmashauri na viwanda vya chai. Nilielekeza viwanda vianze kulipa mapato kwa mujibu wa sheria. Kiasi cha Tsh. 11.7 bilioni zilizokuwa zinadaiwa, zililipwa Tsh. 2 bilioni na kubaki kiasi cha Tsh. 9.6 bilioni. Makampuni ya Uniliver, Kisigo na MTC hadi sasa hayajalipa ni hii inaonesha ni kutotii sheria kwani tangu mwezi Machi, 2020 hadi sasa ni miezi miwili. Jambo hili halijanipendeza hata kidogo, kwani wanaendelea kulipa kwa mtindo wa Memorandum of Understanding (MOU), kitu ambacho hakipo kwenye taratibu. Ninapofikia katika suala la mapato huwa sina mchezo, na hii huwa naona ni dharau. Sasa tarehe 02/06/2020 saa 04:00 asubuhi nawahitaji Wakurugenzi wote wa makampuni haya ya chai bila kukosa, na sitaki kuleta mwakilishi. Mkurugenzi wa Halmashauri, Mwenyekiti, Mkuu wa Wilaya bila TAKUKURU, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa nanyi muwepo bila kukosa, waje watoe maelezo kwanini wameshindwa kulipa ushuru kwa mujibu wa sheria. Wananchi wana matatizo sana kodi na ushuru ndizo zinatufanya tutatue matatizo ya wananchi, lakini naona mnanichezea katika hili. Nasisitiza kuwa, suala la mapato kwa Serikali ya Rais JPM halina mzaha, hivyo tukutane Jumanne tujue mbivu na mbichi. Tafrisi hii ni kukiuka sheria, mimi kama Namba Moja katika Mkoa huu, ni wajibu wangu kusimamia sheria na taratibu zote za nchi kwani mimi ndiye ninamuwakilisha Mheshimiwa Rais, na Serikali haichezewi.
  • Mwisho nawashukuru Madiwani kwa ushirikiano wetu katika kipindi chote nilichokuwepo, wale ambao wanaenda kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi nawatakia kila la heri.

Mwisho Mwenyekiti wa Halmashauri alitoa maombi kwa Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa

  • Tuna Kata 27 Madiwani wote ni wa Chama cha Mapinduzi
  • Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kutoa siku tatu za maombi na siku tatu za kumshukuru Mwenyezimungu
  • Tumepokea fedha na vifaa kwa ajili ya hospitali, tunashuru sana
  • Tunaahidi kumpa kura zetu zote
  • Tumepata bahati ya kuwa na migodi ya madini, tusaidie kusimami katika hili, wachimbaji hawataki kulipa ushuru.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.