• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga Azindua Kampeni Ndogo ya Chanjo ya UVIKO-19

Posted on: July 20th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Iring Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amezindua kampeni ndogo ya chanjo ya UVIKO-19 Mkoani Iringa ambayo ina lengo la kuongeza kasi ya uchanjaji.

Mhe.Sendiga amesema kuwa Mkoa wa Iringa ni moja kati ya mikoa inayotekeleza zoezi la uchanjaji chanjo ya UVIKO-19 ili kuwakinga wananchi dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19. Chanjo za UVIKO-19 zimeidhinishwa na shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya Mapambano ya Ugonjwa wa UVIKO-19. Chanjo hizi zinapunguza uwezekano wa mtu kuambukizwa ugonjwa UVIKO-19 na hata mtu akiambukizwa hupunguza uwezekano wa kulazwa na kufa.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Iringa amesema Mpaka sasa mkoa wa Iringa Umepokea chanjo za aina tano ambazo ni Janssen, Pfizer, Moderna, Sinovac na Sinopharm. Chanjo hizi zimeidhinishwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutumika nchini.

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa, Baada ya Mafanikio makubwa kupatikana katika awamu ya kwanza ya mpango jumuishi harakishi wa uchanjaji chanjo ya UVIKO-19 Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilizindua Awamu ya pili ya mpango shirikishi na harakishi wa uchanjaji chanjo ya UVIKO-19 mnamo tarehe 22 Desemba 2021 Mkoani Arusha. Lengo la mpango huu ni kuongeza kasi ya uchanjaji kuelekea kufikia asilimia 70 ya watanzania ifikapo Desemba 2022.

“Kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari 2022 hadi tarehe 18 Julai 2022 mkoa umepokea chanjo za UVIKO-19 495,307 (Janssen 238035, Pfizer 161650, Sinopharm 51832, Sinovac 31500 na Moderna 12290).  Uchanjaji chanjo ya UVIKO-19, umendelea kufanyika na kwa sasa mkoa unatekeleza kampeni ya uchanjaji chanjo ya UVIKO-19 iliyoanza tarehe 1 Juni 2022 hadi 30 Septemba 2022. Hadi kufikia tarehe 18 Julai 2022 mkoa umechanja jumla ya watu 133,497 sawa na asilimia 19.8 ya walengwa 671,974.” Mhe. Queen Sendiga.

Na hivyo Kuanzia tarehe 20 Julai 2022 hadi kufikia 24 Julai 2022 tutakuwa na kampeni ndogo ya uchanjaji chanjo ya UVIKO-19 inayolenga kuchanja wateja 100,000. Kufikia malengo haya kila halmashauri inatakiwa kuchanja wateja zaidi ya 2500 kwa siku.

Mhe. Queen Sendiga amemaliza kwa kuwahamasisha wananchi wote walio na umri wa miaka 18 na kuendelea ambao bado hawajapata chanjo ya UVIKO-19 wapate chanjo hii katika kipindi hiki cha kampeni. Pia wananchi waliopata dozi ya kwanza wafike katika vituo vya kutolea huduma za chanjo kupata dozi ya pili ili miili yao iweze kuwa na kinga kamili.

Kwa chanjo ya Sinopharm dozi ya pili inatolewa siku 28 baada ya kupata dozi ya kwanza na kwa chanjo ya Pfizer au Moderna dozi ya pili inatolewa kuanzia siku ya 21 hadi 28 baada ya kupata dozi ya kwanza. Kwa sasa mkoa una jumla ya vituo 259 vinavyotoa huduma za chanjo. Pamoja na uchanjaji katika vituo watoa huduma wanatumia huduma za mkoba ili kuwafikia wananchi popote walipo.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.