• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Mwenendo wa Hali ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019 Mkoa wa Iringa

Posted on: November 26th, 2019

Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa ulifanyika Nchini tarehe 24 Novemba, 2019. Idadi ya Halmashauri ambazo zilifanya Uchaguzi huo katika Mkoa wa Iringa ni mbili (2) ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Aidha, Halmashauri tatu (3) za Mji Mafinga, Mufindi DC na Iringa DC hazikufanya Uchaguzi huo kwani wagombea wote wa nafasi zote katika Halmashauri husika walipita bila kupingwa. 

Maeneo yaliyofanya Uchaguzi katika Halmashauri tajwa ni kama ifuatavyo;

  • Halmashauri ya Manispaa ya Iringa 
  • Kata ya Isakalilo
  • Mtaa wa kihodombi A

Ulifanyika Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati ya Mtaa watano (5) (Kundi la Wanawake 2 na Kundi Mchanganyiko 3) ambapo Wagombea wote watano waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).

  • Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo 
  • Uchaguzi wa Wenyeviti wa Vitongoji 6
  • Kitongoji cha Ifiga Ofisini (Katika Kijiji cha Kihesa Mgagao, Kata ya Ng’uruhe)
  • Vitongoji vya Madukani, Uhanyana, Ngugi na Mashariki (Katika Kijiji cha Mtitu, Kata ya Mtitu)
  • Kitongoji cha Lyasa B (katika Kijiji cha Lyasa, Kata ya Image).

Wenyeviti wote sita waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

  • Uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kundi la Wanawake
  • Ulifanyika katika Vijiji vinne (4) vya Mtitu (Kata ya Mtitu), Vitono na Uhambingeto (Katika Kata ya Uhambingeto) na Lyasa (katika Kata ya Image) ambapo jumla ya Wajumbe 32 walichaguliwa. Wajumbe wote 32 waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
  • Uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kundi Mchanganyiko;
  • Ulifanyika katika Vijiji vinne (4)  vya Mtitu, (Kata ya Mtitu), Lyasa (katika Kata ya Image), Vitono na Uhambingeto (Kata ya Uhambingeto) ambapo jumla ya Wajumbe 45 walichaguliwa. Wajumbe wote 45 waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
  • Idadi ya vituo vya kupigia kura:
  • Halmashauri mbili (2) ambazo zilifanya Uchaguzi zilikuwa na jumla ya vituo vya kupigia kura 21 kwa mchanganuo ufuatao:-
  • Halmashauri Manispaa ya Iringa kituo 1
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo vituo 20

Katika uchaguzi huo, jumla ya Viongozi/Wajumbe 88 walichaguliwa katika Halmashauri hizo mbili. Aidha, washindi wote 88 waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM). Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu mkubwa.

Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano,

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa,

Humphrey Kisika.

MUHTASARI WA TAKWIMU ZA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA, 2019 MKOA WA IRINGA 

Muhtasari wa hali halisi ya Wagombea wa Uchaguzi tajwa katika Mkoa wa Iringa ilikuwa kama ifuatavyo;

  • Idadi ya nafasi mbalimbali za Uongozi zilizokuwa zinagombewa ni 10,348
  • Idadi ya Wagombea waliopita bila kupingwa, na waliopita bila kupingwa baada ya Wagombea wengine kukosa sifa wakati wa Uteuzi na Wagombea wengine walioteuliwa kujitoa ni 10,260. Hii ni sawa na 99.15% ya Wagombea wote.
  • Idadi ya nafasi mbalimbali za Uongozi ambazo Uchaguzi wake ulifanyika tarehe 24 Novemba, 2019 ni 88. Hii ni sawa na 0.85% ya wagombea wote.

NB:Jedwali linaloonesha idadi ya Wagombea waliopita bila kupingwa kwa kila nafasi ya Uongozi katika Halmashauri zote tano (5) za Mkoa wa Iringa na waliochaguliwa tarehe 24 Novemba, 2019 ni kama ilivyoamabatishwa. Aidha, Wagombea wote waliopita bila kupingwa na waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).

Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano,

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa,

Humphrey Kisika.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.