• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

RC Hapi awaonya wanaokopesha "fedha za moto"

Posted on: May 7th, 2020

Mkuu wa Mkoa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi aongoza jopo la TAKUKURU kukabidhi magari ya wananchi walioporwa kwa misingi ya dhuluma tarehe Mei 07, 2020.

Mheshiwa Hapi amekabidhi magari hayo kwa wananchi ambao walikopa fedha katika taasisi (SACCOS) ambazo si halali na kusababisha wananchi kushindwa kulipa mikopo kwa kuwazidishia riba na hatimaye kuonekana mkopo haumaliziki na kupelekea kuporwa mali zao.

Akiongea na Wanahabari leo Mheshimiwa Hapi amesema, wananchi wanahitaji fedha kutoka Taasisi mbalimbali za kukopesha, lakini kuna watu wameibuka na kuvunja sheria za nchi na kukopesha bila kufuata sheria, na sehemu kubwa ya mikopo hii haieleweki riba zake zinakokotolewa vipi. Serikali imekuwa imepambana na jambo hili kwa muda mrefu sasa. Wapo wakopeshaji hadi wanachukua kadi za benki kutoka kwa watumishi waliokopa. Mtu anaweza kumaliza mkopo lakini anaambiwa bado deni halijaisha.Hivi karibuni kumekuwa na uhujumu uchumi kupitia vyama mbalimbali vya ushirika, mwanachama anakopa na hataki kurejesha mkopo.

Leo nasimama hapa kueleza wenzetu TAKUKURU walivyofanya kazi nzuri kuweza kuwabana na kurejesha mikopo na magari yaliyoporwa kwa wananchi ambao walikopa fedha za moto.  Magari hayo ni fuso lenye namba T 165 BLW na Toyota Serena (Noah) lenye namba T 311 DDF ambayo yaliporwa tangu mwaka 2017.

Mheshimiwa Hapi aliendelea kusema, ninawahakikishia wananchi kuwa sisi viongozi tuna dhamana kubwa ya kusaidia wananchi katika matatizo yao. Tumerejesha mali za awananchi ambazo zimeporwa kupitia minada feki, mikopo ya moto. Pia kiasi cha Shilingi 3.4 bilioni zimeokolewa kutoka kwa watu waliokopa kwenye  vyama mbalimbali vya ushirika na kushindwa kurejesha. Nawasihi wananchi kuwa makini katika fedha za moto.

Naye Mkuu wa TAKUKURU Iringa ameeliza kuwa wanaendelea na ufuatiliaji wa madeni katika operasheni ili kuweza kuokoa fedha zaidi na kufanya uchunguzi wa masuala mbalimbali.

Pia mwananchi Mwalimu mstaafu (Bi Hadija Mazola) aliyeporwa gari kwa kukopa kiasi cha shilingi milioni mbili na akaweza kulipa kiasi cha shilingi milioni nne, lakini baadaye wakamuambia anadaiwa kiashi cha shilingi milioni nane. Aliposhindwa kulipa deni hilo ndipo akaporwa gari hiyo.

Nao wananchi walioporwa magari hayo waliishukuru Serikali na kuwapongeza kwa kazi wanazofanya. Kwani hawakutegemea kama magari yao yangerejea.

Imetolewa na:

Ofisi ya Habari Mkoa.

 

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.