• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Saratani ya Kizazi kuua Wanawake Iringa

Posted on: April 19th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Saratani ya mlango wa kizazi imekuwa ikichangiwa na kujamiiana katika umri mdogo na kuwa na wapenzi wengi na kusababisha vifo vya wanawake wengi mkoani Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu huria jana.

Masenza alisema kuwa saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa na mambo mengi. “Saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa na vitu vingi ikiwemo kuanza kujamiana katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuwa na ndoa za mitala, kuzaa watoto wengi, na uvutaji wa sigara” alisema Masenza.

Akiongelea dalili za saratani hiyo, alisema kuwa mara nyingi hujitokeza ikiwa imeshasambaa mwilini. Dalili hizo alizitaja kuwa ni kutokwa damu ya hedhi bila mpangilio pamoja na kutokwa damu baada ya kujamiana. Nyingine alizitaja kuwa ni maumivu ya mgongo, miguu na kiuno. Nyingine ni kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa au kokosa hamu ya kula, kutokwa uchafu wa rangi ya kahawia au wenye damu kwenye uke, maumivu ya miguu au kuvimba. “Dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kupatwa na fistula, na uvimbe wa tezi” alisisitiza Masenza.

Mkuu wa mkoa wa Iringa alielezea mkakati utakaotumika katika utoaji chanjo hiyo kuwa ni utaratibu wa kawaida katika vituo vya kutolea huduma za chanjo, baadhi ya shule zitachaguliwa na maeneo katika jamii na chanjo itatolewa kwa njia za huduma za mkoba.

Chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi itatolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali na binafsi bila malipo.

=30=



Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.