• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

Serikali Kuendeleza Biashara Ndogo- RC Masenza

Posted on: March 26th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Serikali imeandaa mkakati wa kuendeleza biashara ndogo kwa lengo la kufikia uchumi unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua maonesho ya wajasiriamali wadogo na wa kati katika uwanja wa mashujaa mjini Mafinga jana.

Masenza alisema kuwa katika nchini nyingi duniani, asilimia kubwa ya pato la watu binafsi linatokana na biashara ndogo na za kati. “Hivyo kuendeleza sekta hii ni mkakati wa kutimiza  malengo ya dira ya maendeleo ya Taifa ni kuwa na uchumi imara unaotegemea  uzalishaji katika viwanda  ifikapo 2025” alisema Masenza. Aidha, aliwataka SIDO kuandaa mkakati wa kuwasaidia wajasiriamali waweze kupata masoko ya kudumu ndani na nje ya nchi.

Akiongelea changamoto ya uingizaji bidhaa kutoka nje, mkuu wa mkoa alisema kuwa uzalishaji wa bidhaa nyingi ndiyo suluhisho la kujitegemea kwa mkoa wa Iringa. Alisema kuwa uzalishaji huo utapunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kuongeza matumizi ya malighafi zinazozalishwa ndani kutumika katika viwanda vya ndani. “Utaratibu huu utasaidia kulinda viwanda vyetu wenyewe bila kutegemea masoko ya nje tu kwa baadhi ya malighafi zetu” alisema mkuu wa mkoa.

“Katika kipindi hiki chenye changamoto za kiuchumi duniani tujitahidi kuzalisha bidhaa kwa wingi na zenye ubora wa hali ya juu ili kuongeza ajira na pato la Taifa. Wananchi wote, wafanyabiashara na viongozi mliobahatika kutembelea maonesho haya, hii ni fursa nzuri ya kuweka miadi na kununua au kuchangia mawazo yenu katika kuboresha bidhaa zetu za hapa nchini, ili kusaidia kujenge msingi imara wa viwanda na uchumi wetu” alisisitiza mkuu wa mkoa.

Maonesho ya wajasiriamali kwa mkoa wa Iringa ni ya kwanza ya aina yake yaliyoandaliwa na T-LED, SIDO, TCCIA, TWCC  kwa kushirikiana na Halmashauri ya mji wa Mafinga.

=30=




Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.