• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

UCHAGUZI WA WANAFUNZI WATAKAOINGIA KIDATO CHA KWANZA 2020 AWAMU YA PILI TAREHE 03/01/2020. Ndugu

Posted on: January 3rd, 2020

TAARIFA YA KATIBU TAWALA WA MKOA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA WANAFUNZI WATAKAOINGIA KIDATO CHA KWANZA 2020 AWAMU YA PILI TAREHE 03/01/2020.

Ndugu

Waandishi wa habari,

Awali ya yote napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wote kwa kuweza kuhudhuria kikao hiki kifupi ambacho ni muhimu kwa Mkoa wetu. Aidha niwape heri ya mwaka mpya 2020.

Ndugu Wanahabari, 

Mtakumbuka kuwa tarehe 14/12/2019 niliwasilisha taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza 2020 ambapo nilieleza kuwa Mwaka 2019 Mkoa wa Iringa ulikuwa na jumla ya watahiniwa 25,325 waliosajiliwa kufanya mtihani wakiwemo wavulana 11,900 na wasichana 13,425 katika shule 493, Kati yao watahiniwa 24,998 (wavulana 11,705 na wasichana 13,293) sawa asilimia 98.7 walifanya mtihani. Watahiniwa 22,130 (wavulana 10,324  wasichana 11,806) sawa na asilimia 88.53 walifaulu mtihani huo. Kiwango hiki cha ufaulu kiliongezeka kwa asilimia 5.3 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka uliopita  ambapo ufaulu ulikuwa ni asilimia  83.23

Mkoa wetu ulishika nafasi ya tatu (3) kitaifa kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara.

Ndugu wanahabari,

Ongezeko la ufaulu lilibua changamoto ya uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa katika shule zetu za sekondari au ujenzi wa shule mpya za Sekondari ili kuweza kuwachukua wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza. Hali iliyosababisha wanafunzi 3480 (Iringa Manispaa-893, Iringa DC-661 na Kilolo-1926) kushindwa kupangwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2020 kutokana na ukosefu wa vyumba vya Madarasa.

Ndugu wanahabari,

Kutokana na changamoto hiyo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri  ziliweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha wanafunzi wote wanajiunga Kidato cha Kwanza kwa wakati. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kukamilisha na kupata vibali vya uanzishaji wa shule za sekondari mpya  ambapo jumla ya shule tatu za sekondari zimepata vibali ambazo ni Mivinjeni iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Shule Mbili za Makifu na Izazi zilizopo katika Halmashauri ya Iringa.

Mkakati Mwingine ni upatikanaji wa nafasi wazi katika shule za Sekondari kwa kutumia vyumba vilivyokuwa vikitumika kwa shughuli nyinginezo na pia kuweza kuomba kibali cha kutumia utaratibu wa wanafunzi kusoma kwa awamu mbili kwa siku  (Double Shift)

 

 

 

Ndugu Wanahabari,

Sasa, napenda kuchukua nafasi hii kutamka rasmi kuwa wanafunzi  wote 3480 (Iringa Manispaa-893, Iringa DC-661 na Kilolo-1926) waliobaki awamu ya kwanza kutokana na upungufu wa miundombinu ya madarasa wamepangiwa  shule ili waanze masomo yao ya kidato cha Kwanza Mwaka 2020 na watapaswa kuripoti katika shule walizochaguliwa ifikapo Jumatatu tarehe 06-01-2020  saa 1.30 asubuhi  siku ambayo shule zitakapofunguliwa na kuanza masomo mara moja.

Baada ya maelezo haya mafupi nina imani taarifa hii itawafikia wananchi wote wa Mkoa wa Iringa kwa kupitia vyombo vyenu vya habari.

     

      Ninawashukuru sana kwa kunisikiliza.

LUCAS KAMBELENJE

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa

IRINGA



 

 

Imetolewa na:

 

Ofisi ya Habari Mkoa,

Humphrey Kisika.

Takwimu za wanafunzi Kidato cha I Awamu ya Pili 2020.docx

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.